Huawei yatoa mafunzo kwa roboti katika maonyesho ya wanafunzi nchini Kenya

(CRI Online) April 10, 2024

Kampuni ya Huawei ya China imetangaza kuwa, darasa la kidijitali linaloitwa DigiTruck linalotoa mafunzo ya ujuzi wa kidijitali kwa jamii maskini barani Afrika, litatoa mafunzo ya papo kwa hapo kwa njia ya roboti katika Maonyesho ya 60 ya Sayansi na Ufundi ya Kenya yaliyoanza Jumanne wiki hii.

Kampuni hiyo imesema katika taarifa yake jana Jumanne kuwa, wanafunzi wa shule za sekondari wanatarajiwa kupata fursa ya kujifunza na kushiriki mafunzo hayo kama sehemu ya shughuli hiyo ya wiki nzima.

Katika taarifa yake hiyo iliyotolea jijini Nairobi, kampuni hiyo imesema inafurahi kuwa sehemu ya shughuli hiyo, ambayo inaendana na ahadi yake ya kuboresha fursa za mafunzo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya.

Maonyesho ya Sayansi na Ufundi ya Kenya ni tukio la kila mwaka linalotumika kuonyesha miradi na mawazo ya ubunifu ya wanafunzi wa shule za sekondari nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha