Nchi za Pembe ya Afrika kukumbwa na wimbi la joto kali

(CRI Online) April 10, 2024

Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa (ICPAC) kulicho chini ya Mamlaka ya Kiserikali kuhusu Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) jana Jumanne kimesema, nchi kadhaa za Pembe ya Afrika zinatazamiwa kukumbwa na wimbi la joto kali kutokana na kuongezeka kwa hali ya joto.

Katika utabiri wake wa karibuni, ICPAC imetabiri kuwa wimbi hilo la joto kali litatokea katika siku zijazo licha ya ukweli kwamba nchi nyingi za eneo hilo zinakabiliwa na mvua kubwa kuliko kawaida wakati wa msimu wa mvua kuanzia mwezi Machi hadi Mei.

ICPAC imetabiri kuwa halijoto inatarajiwa kuongezeka katika maeneo ya kusini mwa Somalia, kusini-mashariki mwa Kenya, eneo la Afar nchini Ethiopia na maeneo ya kaskazini mwa Sudan Kusini. ICPAC pia imeongeza kuwa halijoto ya wastani inatarajiwa kufikia nyuzi joto 32.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha