Li Xi akutana na ujumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2024

Li Xi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni  Katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, akikutana na ujumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazil (PT) unaoongozwa na Rais wake Gleisi Hoffmann mjini Beijing, China, Aprili 10, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Li Xi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, amekutana na ujumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazil (PT) unaoongozwa na Rais wake Gleisi Hoffmann mjini Beijing siku ya Jumatano.

Huku akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Brazil, Li amesema China ingependa kushirikiana na Brazil kuendeleza mawasiliano ya kirafiki katika nyanja mbalimbali na katika ngazi zote, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuzidisha ushirikiano wa kimkakati, na kuhimiza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Brazil kuingia kwenye kiwango kipya.

“CPC inapenda kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano kati ya chama cha CPC na chama cha PT kuzidisha zaidi uhusiano kati ya vyama hivyo” Li amesema.

Kwa upande wake Hoffmann amesema chama cha PT kinapenda kufanya juhudi za pamoja na CPC ili kuimarisha mawasiliano katika ujenzi na utawala wa chama, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha kuunganisha mikakati ya maendeleo na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na kukabiliana kwa pamoja na changamoto za dunia nzima.

Li Xi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni  Katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, akikutana na ujumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazil (PT) unaoongozwa na Rais wake Gleisi Hoffmann mjini Beijing, China, Aprili 10, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Li Xi, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, akikutana na ujumbe wa Chama cha Wafanyakazi cha Brazil (PT) unaoongozwa na Rais wake Gleisi Hoffmann mjini Beijing, China, Aprili 10, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha