Waziri Mkuu wa China Li Qiang ampongeza Bi. Judith Tuluka kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa DRC

(CRI Online) April 11, 2024

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang ameongea kwa njia ya simu na Bi. Judith Suminwa Tuluka, na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Bw. Li Qiang amesema, China na DRC ni washirika wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na kwamba katika miaka ya hivi karibuni, chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping wa China na Rais Felix Tshisekedi wa DRC, urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili unazidi kuimarika, huku ushirikiano na mabadilishano katika sekta mbalimbali yakiongezeka.

Bw. Li amesema serikali ya China inatilia maanani uhusiano kati ya China na DRC, na iko tayari kufanya juhudi pamoja na Bi. Tuluka na serikali ya awamu mpya ya nchi hiyo kutekeleza vizuri makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais hao wawili, kushikilia kuungana mkono katika maslahi makuu ya kila upande, na kuendeleza ushirikiano wa pande mbili wenye ufanisi, ili kufanya matunda ya uhusiano washirika wa kimkakati wa pande zote kati ya China na DRC yanufaishe zaidi watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha