Askari wa kulinda amani wa China nchini DRC wapewa tuzo ya amani ya Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2024

Askari wa kulinda amani wa China wakishiriki hafla ya kutoa tuzo kwenye kambi ya uhandisi ya kikosi cha China nje kidogo ya Bukavu, Mji Mkuu wa jimbo la mashariki la Kivu Kusini, DRC, Aprili 9, 2024. (Kikosi cha 27 cha Kulinda Amani cha China cha MONUSCO/ Xinhua)

BUKAVU, DRC - Kikosi cha 27 cha Kulinda Amani cha China kwenye kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kimepewa tuzo ya amani ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne katika hafla iliyofanyika kwenye kambi ya uhandisi ya kikosi hicho cha China nje kidogo ya Bukavu, mji mkuu wa jimbo la mashariki la Kivu Kusini.

Katika kipindi cha miaka 21 iliyopita, askari wa kulinda amani wa China wamekuwa mfano wa kujitolea na utalaama kupitia majukumu yao, amesema Bintou Keita, mjumbe mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, anayeongoza MONUSCO. Pia ameishukuru serikali ya China kwa kutuma askari wa kulinda amani katika Jimbo la Kivu Kusini tangu Mwaka 2003.

Askari hao wa China wamesaidia kulinda amani na maendeleo katika Kivu Kusini na kutoa mchango mkubwa katika mchakato wa kujiondoa kwa MONUSCO nchini humo, Keita ameongeza, huku akielezea fahari yake kwa askari hao wa China.

Zhao Bin, Balozi wa China nchini DRC amesema, kupitia huduma za matibabu na ujenzi wa barabara, askari hao wa China wametoa mchango katika kudumisha amani na kuongeza urafiki, wakipata sifa kubwa kutoka MONUSCO, serikali ya DRC na watu wa Kivu Kusini.

Ikiwa ni rafiki wa kuaminika na mwenzi wa kimkakati wa pande zote wa DRC, China siku zote imekuwa ikiunga mkono kwa dhati juhudi za DRC katika kulinda mamlaka, usalama na ukamilifu wa ardhi ya nchi hiyo, Zhao amesisitiza, huku akibainisha kuwa China siku zote imekuwa ikifanya kila iwezalo kuisaidia DRC kuimarisha uwezo wake wa kiusalama.

Tangu Septemba 2023, kikosi cha 27 cha askari wa kulinda amani cha China kilichopelekwa, kimetimiza majukumu yao ya kulinda amani mashariki mwa DRC. kikosi cha uhandisi cha China kimeandaa tafiti 13 za kihandisi na kukamilisha miradi 16 kwa kiwango cha juu, huku kikosi cha matibabu kimehudumia wagonjwa wapatao 500, kutoa msaada wa matibabu kwa askari wa MONUSCO walioko Bukavu.

Bintou Keita (Kushoto, mbele), mjumbe mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye anaongoza Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), akipeana mkono na askari wa kikosi cha kulinda amani cha China kwenye kambi ya uhandisi ya kikosi hicho cha China nje kidogo ya Bukavu, mji mkuu wa jimbo la mashariki la Kivu Kusini, DRC, Aprili 9, 2024. (Kikosi cha 27 cha Kulinda Amani cha China cha MONUSCO/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha