Dereva mwanamke wa Nigeria apokewa kwa shamrashamra baada ya safari ya kuendesha gari peke yake barabarani kwa siku 68 kutoka London hadi Lagos

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2024

Gavana wa Babajide Sanwo-Olu wa Jimbo la Lagos (Kulia) akimkabidhi Namba ya Mahsusi ya Gari Pelumi Nubi kwenye mkutano kati ya Gavana na Nubi katika ofisi ya gavana ya Lagos, Marina, Nigeria, Aprili 8, 2024. (Shirika la Habari la Nigeria/ Xinhua)

ABUJA - Pelumi Nubi amewasili katika eneo la kusini-magharibi mwa Nigeria siku ya Jumapili kwenye kituo cha mwisho cha safari yake ya kuendesha gari peke yake barabarani kwa siku 68 kutoka London, Uingereza hadi Lagos, Nigeria akikumbatiwa na ndugu zake, marafiki, maafisa wa serikali na mashabiki wake- ikiashiria mwisho wa tukio hilo ambalo limevuka mipaka na kuhamasisha mioyo.

Mtu huyu anayesafiri kuzunguka dunia na anayeweka picha na video za safari zake mtandaoni mwenye umri wa miaka 28, Januari 30 alianza safari hiyo ya maisha yake, akipitia sehemu nyingi zenye mandhari tofauti, akiwa anaendesha gari lake la kutegemeka, au "rafiki wa safari," ambalo amelipa jina la "Gari Lumi".

Akiendesha gari kupita katika nchi 17, huku akiwa na changamoto, mafanikio na nyakati zisizosahaulika za usafiri, Nubi amesema safari yake hiyo haikuwa safari ya kimwili tu bali ni uthibitisho wa nguvu ya shauku, uhimilivu na kufuata ndoto bila kuchoka.

"Ninajisikia vizuri sana kuwa nyumbani. Kusema kweli, kurudi nyumbani kumekuwa wa kustaajabisha na wa kukaribishwa sana," amesema, huku akishukuru shangwe kutoka kwa mashabiki wake na watu waliokusanyika kwa ajili ya hafla ya kumkaribisha kurudi nyumbani.

Licha ya kukumbana na vikwazo, ikiwa ni pamoja na ajali mbaya katika eneo lisilojulikana mwishoni mwa mwezi Machi, na uharibifu mkubwa wa sehemu ya mbele na kioo cha gari lake, Nubi alisonga mbele bila kukata tamaa, akipata nguvu kutoka kwa uamuzi wake na ujasiri.

Wazazi wake wamesema walikubali safari hiyo kwa sababu amekuwa akionyesha ujasiri tangu Mwaka 2016, na tayari alikuwa ametembelea nchi zaidi ya 80 kabla ya kuanza safari hiyo mwezi wa Januari.

Baba yake Timothy Nubi amesema, kuwasili kwa binti yao huyo kunaashiria "wasiwasi kwa familia umekwisha," akisema safari hiyo ya peke yake ilikuwa kama ndoto mbaya kwa jamaa zake.

Siku ya Jumapili jioni, serikali ya Jimbo la Lagos ilimtangaza Nubi kuwa balozi wake huku ikimpa zawadi ya gari jipya lililoundwa na Kampuni ya magari ya GAC ya China na nyumba mpya kama zawadi.

Pelumi Nubi akiwa katika picha na gari lake jipya kabisa la Kampuni ya magari ya GAC ya China lililotolewa na Gavana Babajide Sanwo-Olu wa Jimbo la Lagos alipomtembelea Gavana huyo katika ofisi ya gavana wa Lagos, Marina, Nigeria, Aprili 8, 2024. (Shirika la Habari la Nigeria/ Xinhua )

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha