EAC yafikiria kuifanya siku ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Ruwanda kuwa Siku ya EAC

(CRI Online) April 11, 2024

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetoa taarifa siku ya Jumanne ikisema kuwa, inafikiria uwezekano wa kuifanya tarehe 7 Aprili ya kila mwaka kuwa Siku ya EAC ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Jumuiya hiyo, naibu katibu mkuu wa EAC Bw. Andrea Aguer Ariik Malueth ametoa ahadi hiyo Jumapili wakati wa hafla ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Bw. Malueth amesema, ombi rasmi litawasilishwa hivi karibuni kwa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo kwa majadiliano kwa kuwa Jumuiya hiyo inachukua nafasi ya uongozi kuhakikisha kuwa yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 hayatatokea tena popote katika eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha