China yapenda kutumia "Mwaka wa Urafiki wa China na DPRK" kuwa fursa ya kuongeza uhusiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2024

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa  Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Choe Ryong Hae, Mjumbe wa Tume Tendaji ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Leba cha   Korea (WPK) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Juu la Umma la Jamhuri ya Umma ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK), mjini Pyongyang, DPRK, Aprili 11, 2024. (Xinhua/ Zhang Ling)

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akifanya mazungumzo na Choe Ryong Hae, Mjumbe wa Tume Tendaji ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Leba cha Korea (WPK) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Juu la Umma la Jamhuri ya Umma ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK), mjini Pyongyang, DPRK, Aprili 11, 2024. (Xinhua/ Zhang Ling)

PYONGYANG - Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China amefanya mazungumzo na Choe Ryong Hae, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Juu la Umma la Jamhuri ya Umma ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK) siku ya Alhamisi, ambapo amesema kuwa urafiki wa jadi kati ya China na DPRK ulianzishwa na kuendelezwa kwa umakini na viongozi waanzilishi wa vyama na nchi hizo mbili.

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping amekuwa akisema mara kwa mara kwamba Chama cha CPC na serikali ya China vinaweka umuhimu mkubwa sana kwenye uhusiano wa jadi wa kirafiki na wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kwamba ni mkakati usioyumba wa China wa kudumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano huo wa pande mbili, Zhao amesema.

Huku akieleza kuwa mwaka huu unatimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na DPRK, Zhao amesema kuwa Katibu Mkuu Xi na Katibu Mkuu wa Chama cha Leba cha Korea (WPK) Kim Jong Un walitumiana salamu za pongezi za mwaka mpya, na kutangaza kwa pamoja Mwaka 2024 kuwa "Mwaka wa Urafiki wa China na DPRK" na kuanzisha shughuli mfululizo.

China ingependa kushirikiana na DPRK katika kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa vyama na nchi hizo mbili, na kutumia "Mwaka wa Urafiki kati ya China na DPRK" kuwa fursa ya kuzidisha mawasiliano ya ngazi ya juu, kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana, kuendeleza mawasiliano kati ya watu na kuimarisha uratibu wa kimkakati, ili kuhimiza uhusiano kati ya China na DPRK uendelee kusonga mbele.

Mawasiliano kati ya vyombo vya utungaji wa sheria yamekuwa sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na DPRK na yamekuwa yakitoa mchango wenye hamasa kwa muda mrefu katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili, Zhao ameeleza.

Kwa upande wake Choe ambaye pia ni Mjumbe wa Tume Tendaji ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya WPK amesema, urafiki ulioimarishwa kwa damu kati ya nchi hizo mbili una historia ndefu na msingi mkubwa, na ni urithi wa pamoja wenye thamani na utajiri wa nchi hizo mbili.

Amesema, chini ya mwongozo wa kimkakati wa Katibu Mkuu Kim na Katibu Mkuu Xi, uhusiano wa kirafiki kati ya DPRK na China umeingia katika zama mpya, ambayo inaonyesha kwa dhati hali ya uhai na kutoweza kuvunjika kwa uhusiano huo wa pande mbili.

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China na Choe Ryong Hae, Mjumbe wa Tume Tendaji ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Leba cha Korea (WPK) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Juu la Umma la Jamhuri ya Umma ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK), wakishuhudia hafla ya  kusaini nyaraka za ushirikiano katika nyanja mbalimbali, zikiwemo za kusameheana visa za kidiplomasia na za watumishi wa umma, kutafsiriana na uchapishaji wa vitabu maarufu , karantini ya forodha, redio na televisheni, na uwasilishaji wa vifurushi kwa njia ya posta baada ya mazungumzo yao mjini Pyongyang, DPRK, Aprili 11, 2024. (Xinhua/ Zhang Ling)

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China na Choe Ryong Hae, Mjumbe wa Tume Tendaji ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Leba cha Korea (WPK) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Juu la Umma la Jamhuri ya Umma ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK), wakishuhudia hafla ya kusaini nyaraka za ushirikiano katika nyanja mbalimbali, zikiwemo za kusameheana visa za kidiplomasia na za watumishi wa umma, kutafsiriana na uchapishaji wa vitabu maarufu, karantini ya forodha, redio na televisheni, na uwasilishaji wa vifurushi kwa njia ya posta baada ya mazungumzo yao mjini Pyongyang, DPRK, Aprili 11, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha