

Lugha Nyingine
Mji wa Vilnius, Lithuanian wawa mwenyeji wa Mkutano wa Mpango wa Bahari Tatu
Washiriki wakihudhuria Mkutano wa Mpango wa Bahari Tatu huko Vilnius, Lithuania, Aprili 11, 2024. (Ikulu ya Lithuania/Xinhua)
VILNIUS - Mkutano wa kilele wa Mpango wa Bahari Tatu (3SI) umefanyika Vilnius, Lithuania siku ya Alhamisi, kwa lengo la kuboresha muunganisho wa miundombinu ya usafirishaji, kuwa na vyanzo mbalimbali vya nishati, na kujenga miundombinu himilivu ambapo wakati akiongoza mkutano wa wajumbe wote wa mkutano huo Rais Gitanas Nauseda wa Lithuania amesema kuwa mkutano huo unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika nyanja za matokeo halisi ya mchakato wa upanuzi wa Umoja wa Ulaya (EU).
"Shukrani kwa Mpango wa Bahari Tatu, tunatilia mkazo zaidi katika uhimilivu wa kikanda wa nafasi ya mtandao wa intaneti, ulinzi wa miundombinu muhimu, na unyumbulifu wa kijeshi" amesema.
Mkutano huo umepitisha tamko la pamoja.
Mpango wa Bahari Tatu (3SI) ni muundo wa ushirikiano ulioanzishwa Agosti 2016 na nchi wanachama 12 wa EU ambazo ni Austria, Bulgaria, Croatia, Jamhuri ya Czech, Estonia, Hungary, Latvia, Lithuania, Poland, Romania, Slovakia na Slovenia.
Washiriki wakihudhuria Mkutano wa Mpango wa Bahari Tatu huko Vilnius, Lithuania, Aprili 11, 2024. (Ikulu ya Lithuania/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma