

Lugha Nyingine
Ethiopia yapata dola za Marekani zaidi ya milioni 600 kutokana na mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo katika muda wa miezi minane
Serikali ya Ethiopia imetangaza siku ya Alhamisi kwamba imepata dola za kimarekani milioni 617 kutokana na mauzo yake ya nje ya bidhaa maalum za kilimo katika muda wa miezi minane.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Wizara ya Biashara na Ushirikiano wa Kikanda ya Ethiopia, imesema mapato hayo yametokana na mauzo ya nje ya bidhaa zinatiliwa mkazo na wizara hiyo kama vile soya, maharage mekundu, na ufuta.
Takwimu kutoka wizara hiyo zinaonyesha kuwa, mapato yaliyoripotiwa ya mauzo ya nje yameongezeka kwa dola za Kimarekani takriban milioni 80 ikilinganishwa na kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha uliopita wa 2022/23.
Wizara hiyo imesema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa mauzo ya nje ya bidhaa kuu za kilimo pamoja na ongezeko la pato la mbegu za ufuta nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma