Kenya yazindua mpango wa kukabiliana na ajira ya watoto katika sekta ya kahawa na chai

(CRI Online) April 12, 2024

Kenya imezindua mradi utakaokomesha ajira ya watoto katika sekta ya kahawa na chai nchini humo.

Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi na Hifadhi ya Jamii ya Kenya, Bi Florence Bore amesema, mpango huo unaoitwa “Hatua ya kuharakisha kukomesha ajira ya watoto katika mnyororo wa ugavi barani Afrika”, utatekelezwa katika miaka mitano ijayo kwenye kaunti 4 za vijijini ambako ajira ya watoto ni jambo la kawaida katika sekta ya kilimo.

Bi Bore amewaambia wanahabari huko Nairobi kwamba mradi huo utaongeza juhudi na nia ya serikali ya kulinda hatma za watoto.

Ameongeza kuwa mradi huo pia utatoa mchango wa kusaidia Kenya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG 8) kuhusu kukomesha ajira ya watoto itakapofika mwaka 2025.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha