Uingereza yafungua milango kustawisha biashara ya maua ya Afrika Mashariki kupitia sera ya kufuta ushuru

(CRI Online) April 12, 2024

Uingereza imeruhusu nchi za kanda ya Afrika Mashariki kuuza maua katika nchi hiyo bila ya kutozwa ushuru hadi mwaka 2026.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana mjini Nairobi, Kenya, Ubalozi wa Uingereza nchini Kenya umesema, nchi hiyo imeondoa kwa muda ushuru wa kimataifa kwa maua, ili kurahisisha biashara na kuleta nafuu zaidi kwa wakulima wa maua katika Afrika Mashariki na nchi nyingine.

Taarifa hiyo imesema, idadi kubwa ya maua isiyo na kikomo inaweza kusafirishwa nchini Uingereza bila ya kulipishwa ushuru, hata kama yakipitia nchi ya tatu.

Nchi za Afrika Mashariki zinazotarajiwa kufaidika na hatua hiyo ya Uingereza ni Kenya, Ethiopia, Rwanda, Tanzania na Uganda.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha