

Lugha Nyingine
Madaktari wa China watoa huduma ya bila malipo ya matibabu kwa jamii nchini Sudan Kusini
Madaktari wa China wametoa huduma za matibabu bila malipo kwa wakazi wa eneo la Nakuten Korok, lililopo Rajaf Payam, kaskazini mwa Jimbo la Juba nchini Sudan Kusini.
Wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo ya tumbo, magua na kutokwa vipele mwilini tangu mwezi Machi mwaka huu, lakini hawakuweza kupata matibabu sahihi mpaka madaktari wa kikosi cha 11 cha Kulinda amani Nchini Sudan Kusini cha China walipotembelea eneo hilo.
Madaktari hao wa Kikosi cha walinzi wa Amani wa China katika Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) walipendekeza kuanzisha kambi ya matibabu baada ya kuona hali mbaya ya wakazi wa huko.
Katibu wa Kijiji cha Nakituen Korok Kusini, Gabriel Ladu, amewapongeza askari wa kulinda Amani wa China na timu ya madaktari kwa kutoa huduma inayohitajika ya matibabu kwa wakazi wa jamii hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma