Zhao Leji akutana na Kiongozi Mkuu wa DPRK, Kim Jong Un

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 15, 2024

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akikutana na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Leba cha Korea (WPK) ambaye pia ni Rais wa Kamati ya Kitaifa ya Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK) mjini Pyongyang, DPRK, Aprili 13, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)

PYONGYANG - Zhao Leji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, ambaye ameongoza ujumbe wa chama na serikali ya China kwenye ziara rasmi ya nia njema katika Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK) amekutana na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Leba cha Korea (WPK) ambaye pia ni Rais wa Kamati ya Kitaifa ya DPRK siku ya Jumamosi ambapo amewasilisha salamu za kutakia mema na kila la kheri kutoka kwa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.

Zhao, ambaye pia ni mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC amesema akiwa ameteuliwa na Xi na Kamati Kuu ya CPC, anaongoza ujumbe wa chama na serikali ya China kufanya ziara rasmi ya kirafiki nchini DPRK na kushiriki kwenye sherehe za ufunguzi wa "Mwaka wa Urafiki wa China na DPRK," na kwamba alipokelewa kwa ukarimu na furaha na WPK na serikali ya DPRK.

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na DPRK, na miaka hiyo 75 iliyopita imedhihirisha ujirani mwema na urafiki huku nchi hizo mbili zikisimama bega kwa bega, zikipigana pamoja na kuchangia mustakabali wa pamoja na kutafuta maendeleo kwa pamoja, amesema.

Zhao amesema, katika hali mpya ya sasa, China inapenda kujiunga na DPRK kusukuma uhusiano kati ya nchi mbili kuelekea maendeleo zaidi kwa kufuata nia ya juu ya viongozi wakuu wa vyama na nchi hizo mbili na matarajio ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili.

Zhao ameeleza kuwa urafiki kati ya China na DPRK, ulioanzishwa na kuendelezwa kwa makini na wanamapinduzi waanzilishi wa vyama na nchi hizo mbili, umestahimili majaribu mbalimbali ya mabadiliko ya hali ya kimataifa na ni mali yenye thamani kubwa kwa nchi hizo mbili.

Zhao amesema, CPC na serikali ya China siku zote inautendea uhusiano kati ya China na DPRK kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na kudumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano wa jadi wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na DPRK ni sera ya China inayotekelezwa kithabiti kabisa.

Amesema China ingependa kuimarisha uratibu katika maendeleo na kuzidisha ushirikiano wa pande mbili na DPRK, na kuendelea kuongeza maendeleo endelevu ya uhusiano kati ya China na DPRK.

Kwa upande wake Kim amemwomba Zhao kufikisha salamu zake za dhati na za kutakia kila la kheri kwa Xi.

Kim amesema kuwa kuteuliwa na Katibu Mkuu Xi na Kamati Kuu ya CPC, ziara ya ujumbe wa chama na serikali ya China nchini DPRK na kushiriki kwenye sherehe za ufunguzi wa "Mwaka wa Urafiki wa DPRK na China" kunaonyesha vya kutosha urafiki wa Katibu Mkuu Xi juu ya uhusiano wa DPRK na China na kuonyesha kwa nguvu msingi imara na usioweza kuvunjika wa uhusiano huo wa pande mbili.

Kim ametoa pongezi zake za dhati juu ya mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana katika mambo ya kijamaa ya China chini ya uongozi madhubuti wa Katibu Mkuu Xi na CPC.

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akikutana na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Leba cha Korea (WPK) ambaye pia ni Rais wa  Kamati ya Kitaifa ya Jamhuri ya Wtu ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK) mjini Pyongyang, DPRK, Aprili 13, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, akikutana na Kim Jong Un, Katibu Mkuu wa Chama cha Leba cha Korea (WPK) ambaye pia ni Rais wa Kamati ya Kitaifa ya Jamhuri ya Watu ya Kidemokrasia ya Korea (DPRK) mjini Pyongyang, DPRK, Aprili 13, 2024. (Xinhua/Liu Weibing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha