

Lugha Nyingine
Raia mmoja wa China auawa, mwingine kujeruhiwa katika shambulizi la halaiki la kuchoma visu kwenye jengo la maduka mjini Sydney, Australia
Mwanamke akiweka maua nje ya Jengo la Maduka la Westfield kwenye Makutano ya Bondi mjini Sydney, Australia, Aprili 14, 2024. (Xinhua/Ma Ping)
SYDNEY - Raia mmoja wa China ameuawa na mwingine kujeruhiwa katika shambulizi la halaiki la kuchoma visu katika jengo la maduka mjini Sydney, Australia, Ubalozi mdogo wa China huko Sydney umesema siku Jumapili ambapo mamlaka za Australia zimethibitisha habari hiyo kwa ubalozi na balozi ndogo za China nchini humo baada ya ujumbe huo wa China kujaribu kupata ukweli wa kutokea kwa tukio hilo kutoka vyanzo mbalimbali.
Ubalozi na balozi ndogo za China nchini Australia zitaendelea kuwasiliana na familia za waathirika, idara zinazohusika za China na upande wa Australia ili kutoa usaidizi kikamilifu kwa kazi zinazofuata.
Watu sita wameuawa katika shambulizi hilo lililotokea kwenye Jengo la Maduka la Westfield katika eneo la Makutano ya Bondi Jumamosi mchana. Wengine 12 wamelazwa katika hospitali mbalimbali za Sydney.
Mshambuliaji huyo, aliyetambuliwa na polisi kwa jina la Joel Cauchi mwenye umri wa miaka 40, amepigwa risasi na polisi katika jengo hilo.
Polisi walisema mapema Jumapili kwamba Cauchi alikumbwa na matatizo ya afya ya akili na hakuna taarifa za kijasusi zinazoonesha kuwa shambulizi hilo linahusiana na itikadi kali.
Polisi wakifanya kazi nje ya Jengo la Maduka la Westfield kwenye Makutano ya Bondi mjini Sydney, Australia, Aprili 14, 2024. (Xinhua/Ma Ping)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma