Chansela wa Ujerumani apongeza ushirikiano wa teknolojia ya hidrojeni kati ya Ujerumani na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 15, 2024

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz akitembelea Kampuni ya Bosch Hydrogen Powertrain Systems ya Chongqing katika Wilaya ya Jiulongpo ya Mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Aprili 14, 2024. (Xinhua/Huang Wei)

CHONGQING – Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema siku ya Jumapili kwamba amefurahishwa na ushirikiano kati ya kampuni za Ujerumani na China katika sekta ya teknolojia ya hidrojeni, na kwamba Ujerumani inapenda kuendelea kuzidisha mawasiliano ya kirafiki kati yake na China na kusukuma ushirikiano wa pande mbili katika ngazi mpya.

Scholz siku ya Jumapili alitembelea kampuni yenye ubia wa China na Ujerumani na mradi wa ushirikiano wa utafiti wa kisayansi kati ya China na Ujerumani kuhusu usimamizi wa maji, na maeneo mengine, baada ya kuwasili mapema siku hiyo katika mji wa Chongqing kuanza ziara yake rasmi ya siku tatu nchini China.

Akiwa kwenye kampuni ya Bosch Hydrogen Powertrain Systems ya Chongqing, Scholz amefahamishwa kuhusu vifaa vya nishati ya hidrojeni inayotumiwa na treni na mchanganyiko wa seli za mafuta zinazotumika kuendesha treni, na kupata uzoefu wa kazi ya kuunganisha sehemu za moduli za nishati ya seli za hidrojeni.

Scholz amesema maendeleo ya teknolojia ya kampuni hiyo na kasi ya ujenzi wa kiwanda ni ya kuridhisha.

Scholz ameambatana na wawakilishi waandamizi wa kampuni kadhaa maarufu za Ujerumani, zikiwemo Siemens, Bayer, Mercedes-Benz, BMW, na Zeiss.

Kampuni zaidi ya 5,000 za Ujerumani zinafanya biashara zao nchini China – nchi ambayo imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Ujerumani kwa miaka mingi.

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz akifahamishwa kuhusu mradi wa ushirikiano wa utafiti wa kisayansi kati ya China na Ujerumani kuhusu usimamizi wa maji huko Jiangbeizui, Mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Aprili 14, 2024. (Xinhua/Huang Wei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha