Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa shinikizo la kimataifa kusitisha mapigano Sudan

(CRI Online) April 16, 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kuwepo kwa shinikizo la kimataifa ili kusitisha mapigano nchini Sudan, mwaka mmoja baada ya mgogoro wa kijeshi kati ya pande mbili.

Akiongea na wanahabari mwaka mmoja baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya vikosi vya Jeshi la serikali ya Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), Bw. Guterres amesema njia pekee ya kuondokana na hali hii ya kutisha ni suluhu ya kisiasa. Ameongeza kuwa katika wakati huu muhimu, mbali na uungaji mkono wa kimataifa kwa ajili ya misaada, unahitajika msukumo wa kimataifa wa kusitisha mapigano nchini Sudan na kufuatiwa na mchakato wa amani.

Amesema kinachoendelea nchini Sudan siyo tu ni zaidi ya mgogoro kati ya pande mbili zinazopigana, bali pia ni vita inayoendeshwa dhidi ya watu wa Sudan, ambao maelfu yao wameuawa na wengine wengi kuachwa na njaa kali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha