Kenya yazindua kituo cha kuhimiza uwekezaji wa ndani na nje ya nchi

(CRI Online) April 16, 2024

Kenya imezindua kituo cha kibiashara na jukwaa la kidijitali ikilenga kuhimiza uwekezaji wa ndani na nje ya nchi nchini humo.

Katibu wa kudumu katika wizara ya uwekezaji, biashara na viwanda ya nchi hiyo, Bi Rebecca Miano, ametangaza mpango huo unaojulikana kama kituo cha uungaji mkono cha biashara cha Karibu, ambao ni pamoja na ofisi halisi zilizoko kote nchini Kenya na tovuti inayotoa huduma mbalimbali ikiwemo uungaji mkono wa ushauri kuhusu uwekezaji, uzalishaji na sera za kibiashara.

Bi Miano amewaambia wanahabari huko Nairobi, kwamba kituo hicho kinatoa habari halisi kwa makampuni na kufanya mawasiliano ya karibu na idara za serikali juu ya mambo ya uwekezaji, viwanda na biashara.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha