China na Tanzania zaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 16, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania, jijini Dar es Salaam, Tanzania, Aprili 15, 2024. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM - China na Tanzania zimefanya hafla ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili siku ya Jumatatu katika mji wa bandari wa Dar es Salaam.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba na Balozi wa China nchini humo, Chen Mingjian, pamoja na Wachina wanaoishi nchini Tanzania na maofisa wa serikali ya Tanzania.

Maonyesho ya picha yaliyofanyika pamoja na hafla hiyo, yaliyoandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Tanzania na Shirika la Habari la China, Xinhua, yakionyesha ushirikiano wenye matokeo halisi kati ya nchi hizo mbili katika miaka 60 iliyopita.

Akihutubia hafla hiyo, Makamba amesema urafiki kati ya nchi hizo mbili umehimili majaribu ya wakati na uhusiano huo umeimarika zaidi leo.

Kwa upande wake Balozi Chen amesema miaka 60 iliyopita imeashiria kipindi cha mshikamano na umoja kati ya China na Tanzania, ambacho kimekuwa na ushirikiano wa dhati, maendeleo kwa pamoja na mabadilishano ya mawazo, pamoja na kuungana mkono.

Amesema katika miaka ya 60 ya karne iliyopita, wakati harakati za ukombozi wa kitaifa zikipamba moto barani Afrika, China ilisimama kidete na Tanzania na nchi nyingine za Afrika na kujenga urafiki mkubwa nazo.

Tarehe 26 Aprili, 1964, Jamhuri ya Watu wa China na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania January Makamba (wa pili kushoto, mbele), Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian (wa kwanza kushoto, mbele) na washiriki wengine wakitembelea maonesho ya picha kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili jijini Dar es Salaam, Tanzania, Aprili 15, 2024. (Ubalozi wa China nchini Tanzania/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha