Rais Xi akutana na Chansela wa Ujerumani Scholz, akitoa wito wa kupata mafanikio ya pande zote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa  la Diaoyutai mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz siku ya Jumanne kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, akitoa wito kwa pande hizo mbili kuendeleza ushirikiano wenye sifa maalumu ya kunufaishana kwa pande zote ili kupata maendeleo kwa pamoja. Huku akisisitiza kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Ujerumani, Rais Xi amesema katika miaka 10 iliyopita, ingawa mabadiliko makubwa yanatokea katika hali ya kimataifa, uhusiano kati ya China na Ujerumani umeendelea kwa hatua madhubuti, na ushirikiano wa pande mbili umeimarishwa na kuzidishwa katika sekta mbalimbali, ukitoa msukumo kwa maendeleo ya nchi zote mbili.

"Kwa hivi sasa, mabadiliko ambayo hayajapata kuonekana katika miaka mia moja iliyopita yanazidi kuwa kasi kote duniani, na jamii za binadamu zinakabiliwa na hatari na changamoto zinazoongezeka. Matatizo haya hayawezi kutatuliwa bila ushirikiano wa nchi kubwa,” Rais Xi amesema.

Rais Xi amesisitiza kuwa China na Ujerumani zimetoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, na nchi hizo mbili hazina mgongano wa maslahi ya kimsingi kati yao, na kila upande hauna tishio la usalama kwa upande mwingine.

Rais Xi ameeleza kuwa minyororo ya viwanda na usambazaji wa bidhaa ya China na Ujerumani ina uhusiano mkubwa, na masoko ya nchi hizo mbili yanategemeana sana. Amesema, ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Ujerumani si "hatari," bali ni uhakikisho kwa uhusiano thabiti wa pande mbili na fursa kwa siku za baadaye.

Kuna uwezo mkubwa wa kifursa utakaotumiwa ipasavyo kwa ajili ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote katika sekta za jadi za mashine na magari, na maeneo mapya ya kuhamia katika maendeleo ya kijani, maendeleo ya kidijitali na akili mnemba, Rais Xi amesema.

Rais Xi ameeleza kuwa China na Ujerumani zina maelewano mengi kuhusu suala la kuwepo kwa ncha nyingi duniani, amedhihirisha kuwa hali halisi ya kuwepo kwa ncha nyingi duniani, kimsingi, ni kuwepo kwa dunia moja ambapo nchi zenye ustaarabu tofauti, mifumo tofauti na kufuata njia tofauti za maendeleo zinaheshimiana na kuishi pamoja kwa amani.

Kwa upande wake, Scholz amesisitiza kuwa uhusiano wa Ujerumani na China sasa uko katika hali nzuri na kwamba nchi hizo mbili zimekuwa na mawasiliano ya karibu katika ngazi zote na sekta zote.

Amesema, pande hizo mbili zimefanikiwa kufanya mashauriano na majadiliano ya ngazi juu baina ya serikali kuhusu masuala ya kimkakati na mambo ya fedha, na zitafanya mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabianchi na kuhamia katika maendeleo ya kijani.

Baada ya mkutano huo, Rais Xi na Chansela Scholz walifanya matembezi na kula chakula cha mchana pamoja, ambapo walibadilishana zaidi mawazo juu ya masuala mbalimbali. 

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Chansela Olaf Scholz wa Ujerumani kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz wakiwa wanatembea pamoja mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz wakiwa wanatembea pamoja mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz wakiwa katika picha ya pamoja mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz wakiwa katika picha ya pamoja mjini Beijing, China, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha