Pato la Taifa la China laongezeka kwa asilimia 5.3 katika robo ya kwanza ya Mwaka 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2024

Roboti zikionekana kwenye mstari wa kuunganisha sehemu za magari wa Kiwanda cha Magari cha Kampuni ya Voyah, ambayo ni chapa ya kifahari ya China ya magari yanayotumia umeme, huko Wuhan, Mkoa wa Hubei, China, Aprili 1, 2024. (Xinhua/Xiao Yijiu)

Roboti zikionekana kwenye mstari wa kuunganisha sehemu za magari wa Kiwanda cha Magari cha Kampuni ya Voyah, ambayo ni chapa ya kifahari ya China ya magari yanayotumia umeme, huko Wuhan, Mkoa wa Hubei, China, Aprili 1, 2024. (Xinhua/Xiao Yijiu)

BEIJING - Takwimu kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zilizotolewa Jumanne zimeonyesha kuwa, pato la Taifa la China (GDP) limeongezeka kwa asilimia 5.3 katika robo ya kwanza ya Mwaka 2024, na kufikia yuan trilioni 29.63 (kama dola trilioni 4.17 za Kimarekani).

Kwa robo mwaka, uchumi huo uliongezeka kwa asilimia 1.6 katika miezi mitatu ya mwanzo.

"Maendeleo yenye sifa bora ya China yamepata mafanikio mapya katika robo ya kwanza. Uchumi wa taifa umeendelea kuimarika na umekuwa na mwanzo mzuri," Sheng Laiyun, Naibu Mkurugenzi wa NBS, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Sheng ametaja mambo mazuri katika kipindi hicho kama vile kuongezeka kwa mahitaji ya uzalishaji, kutuliza kwa ajira na bei ya bidhaa, na kuongezeka kwa imani ya soko.

"Mambo haya yanayochochea ufufukaji wa uchumi yanazidi kuongezeka na kuimarika, yakiweka msingi mzuri wa ukuaji wa mwaka mzima," amesema Sheng.

Sheng amesema kasi nzuri ya ongezeko la pato hilo la uchumi katika robo ya kwanza inahusiana na utekelezaji wa sera za kuunga mkono kutoka serikali na kuimarika kwa nguvu za udhibiti mkubwa wa uchumi.

Pato la Taifa la China lilikua kwa asilimia 5.2 mwaka jana na China imelenga ukuaji wake wa uchumi wa mwaka mzima kwa karibu asilimia 5 katika Mwaka 2024.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha