China yatoa wito kwa pande zote za Libya kuendelea kuhimiza mchakato wa kisiasa kwa njia ya mazungumzo

(CRI Online) April 17, 2024

Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesema China inatoa wito kwa pande zote za Libya kuzingatia kulinda maslahi ya taifa, na kuendelea kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo na kuhimiza maendeleo ya mchakato wa kisiasa.

Balozi Dai Bing ametoa wito huo kwenye mkutano wa baraza la usalama la umoja huo kuhusu suala la Libya, ambapo amesema kuwa hivi karibuni pande zote za Libya ziliendelea kufanya mazungumzo kuhusu mchakato wa uchaguzi na kufikia makubaliano mengi.

“China inaunga mkono juhudi za mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Bw. Abdoulaye Bathily, na inatoa wito kwa ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya kutekeleza majukumu yake” amesema.

China pia imetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kufuatilia maombi ya Libya na kuheshimu ukamilifu wa mamlaka na ardhi ya Libya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha