IMF yaongeza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa Dunia Mwaka 2024 hadi kufikia asilimia 3.2

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2024

Picha hii iliyopigwa Aprili 16, 2024, ikionyesha makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

Picha hii iliyopigwa Aprili 16, 2024, ikionyesha makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Jumanne limeongeza makadirio yake ya ukuaji wa uchumi duniani mwaka 2024 hadi asilimia 3.2, ikiwa ni asilimia 0.1 juu zaidi kuliko makadirio yake ya mwezi Januari, ripoti mpya ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia (WEO) inasema.

Pierre-Olivier Gourinchas, mchumi mkuu na mkurugenzi wa Idara ya Utafiti ya IMF, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari katika kipindi cha Mikutano ya Majira ya Mchipuko ya IMF na Benki ya Dunia Mwaka 2024 kuwa, licha ya makadirio hayo yasiyotia matumaini, uchumi wa Dunia unaendelea kuwa unyumbufu mkubwa, huku ukuaji wa kasi na mfumuko wa bei ukipungua haraka kama ulivyopanda.

"Viashiria vingi vinaendelea kutokana na sera nzuri za kifedha."

Ingawa athari za kiuchumi zinazotokana na misukosuko ya miaka minne iliyopita zimepungua, IMF inakadiria kuwa kutakuwa na athari zaidi kwa nchi zinazoendelea zenye kipato cha chini, ambazo nyingi bado zinahangaika kubadili mwelekeo kutoka kwenye janga la UVIKO-19 na misukosuko ya gharama za maisha, amesema.

IMF inatarajia uchumi wa nchi zilizoendelea kukua kwa asilimia 1.7 katika Mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2 kutoka kwenye makadirio yake ya Januari. Uchumi wa Marekani utaongezeka kwa asilimia 2.7 mwaka 2024 na kupungua kwa asilimia 1.9 mwaka 2025. Uchumi wa eneo linalotumia sarafu ya Euro utaongezeka kwa asilimia 0.8 mwaka 2024, na kuongezeka zaidi hadi asilimia 1.5 mwaka 2025.

IMF inatarajia uchumi wa nchi zenye masoko yanayoibukia na zile zinazoendelea, utakua kwa asilimia 4.2 mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.1 kutoka kwenye makadirio yake ya Januari. Makadirio ya IMF yanaonyesha kuwa uchumi wa China utakua kwa asilimia 4.6 mwaka 2024.

Licha ya maendeleo hayo yanayokaribishwa, Gourinchas amebainisha kuwa changamoto nyingi zinaendelea kuwepo, na hatua madhubuti zinahitajika.

Mwanauchumi mkuu huyo wa IMF amesema kuwa bei ya mafuta imekuwa ikipanda hivi karibuni kwa sehemu kutokana na mvutano wa siasa za kijiografia na mfumuko wa bei wa huduma unaendelea kuwa juu.

Ripoti hiyo inaonyesha hatari kadhaa za kuufanya uchumi kwenda chini: kupanda kwa bei kutokana na mivutano ya siasa za kijiografia, ikiwa ni pamoja na mgogoro wa Ukraine na mgogoro wa Gaza na Israel, kunaweza, pamoja na kuendelea kwa mfumuko wa bei ambapo soko la ajira bado ni ngumu, kuongeza matarajio ya kiwango cha riba na kupunguza bei za mali.

Watu wakitembea kuyapita makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Liu Jie)

Watu wakitembea kuyapita makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, D.C., Marekani, Aprili 16, 2024. (Xinhua/Liu Jie)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha