Botswana yatoa wito wa dhamira ya pamoja katika maendeleo ya teknolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2024

David Zhang, Mkurugenzi Mkuu wa Tawi la Botswana la Kampuni ya Teknolojia ya Huawei, akizungumza kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Simu wa Huawei 2024 huko Gaborone, Botswana, Aprili 16, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE – Serikali ya Botswana imesisitiza tena umuhimu wa habari, teknolojia, na kujifunza katika kuleta mafanikio ya uchumi, na kutoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano zaidi kati ya washikadau.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Simu wa Huawei 2024 huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana, Waziri wa Mawasiliano, Ujuzi na Teknolojia wa Botswana, Thulagano Merafe Segokgo ametoa wito wa dhamira ya pamoja kutoka kwa wadau katika kutumia teknolojia kwa ajili ya kuboresha jamii.

Amesema Botswana inafuata ajenda ya mageuzi ya kidijitali na mabadiliko ya mawazo ambayo inalenga kuendeleza na kuingiza teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika sekta zote za uchumi.

Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa TEHAMA inakuwa zana ya kila mahali na ya lazima, siyo tu kwa sekta fulani pekee, lakini iliyojumuishwa katika muundo wa shughuli zote za kiuchumi, Segokgo amesema.

Kwa mujibu wa waziri hiyo, mbinu ya kimkakati ya Botswana inasisitiza dhamira yake ya kutumia teknolojia kama kichocheo cha uvumbuzi, ufanisi na maendeleo endelevu katika nyanja zake zote za uchumi.

David Zhang, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Teknolojia ya Huawei nchini Botswana, amesema kampuni hiyo imedhamiria kuboresha uwezo wake wa mifumo ya uuzaji na huduma kwa kuboresha michakato na zana za teknolojia ya habari.

"Huawei inafurahi kukaribisha washirika zaidi kusaidia mageuzi ya kidijitali na ya teknolojia za akili bandia ya kampuni ndogo na za kati ili kufikia ukuaji wa pamoja katika soko la usambazaji na biashara," amesema Zhang.

Zhang pia ametoa wito kwa wadau kuchangia ufahamu wao na kujenga ushirikiano mpya ambao utaunda mustakabali wa mawasiliano ya simu.

Waziri wa Mawasiliano, Ujuzi na Teknolojia wa Botswana Thulagano Merafe Segokgo (wa pili, kulia) na wawakilishi kutoka Kampuni ya Teknolojia ya Huawei wakishiriki kwenye hafla ya kuzindua bidhaa na suluhisho za teknolojia za Huawei kwenye Mkutano wa Mawasiliano ya Simu wa Huawei 2024 huko Gaborone, Botswana, Aprili 16, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha