UNICEF: Asilimia zaidi ya 90 ya watoto wenye umri wa kuanza shule wamenyimwa haki ya elimu kutokana na mapigano

(CRI Online) April 17, 2024

Makadirio mapya ya Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), yanaonesha kuwa mapigano yaliyodumu kwa mwaka mmoja kati ya jeshi la serikali ya Sudan (SAF) na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) yamesababisha asilimia 90 ya watoto milioni 19 waliofikia umri wa kwenda shule nchini humo kushindwa kwenda shule.

Shirika hilo limetoa taarifa ikisema Sudan sasa inakabiliwa na msukosuko mkubwa zaidi wa elimu duniani, na ukatikaji wa elimu unaoendelea utasababisha msukosuko zaidi kwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa tawkimu rasmi zilizotolewa na wizara ya elimu ya juu ya Sudan, vita hivyo vimesababisha vyuo zaidi ya 100 vya umma na binafsi kufungwa, na kuharibu idadi kubwa ya vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha