Waziri Mkuu wa China afanya kongamano na wanunuzi kutoka nchi za nje katika Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya kongamano na wanunuzi kutoka nchi za nje wanaoshiriki kwenye Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 17, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya kongamano na wanunuzi kutoka nchi za nje wanaoshiriki kwenye Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Aprili 17, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

GUANGZHOU - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amefanya kongamano na wanunuzi kutoka nchi za nje wanaoshiriki Maonyesho ya 135 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, siku ya Jumatano ambapo wawakilishi wa wanunuzi hao wamezungumza juu ya uzoefu wao katika kuimarisha ushirikiano na China kupitia maonyesho hayo, wakibainisha kwamba maonyesho hayo kwa muda mrefu yamekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza mawasiliano ya kibiashara na uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi nyingine.

Wawakilishi hao wamesema wana imani kubwa na matarajio kwa maendeleo ya uchumi wa China na kwamba wanapenda kuyachukulia maonyesho hayo kama jukwaa la kuendelea kupanua biashara nchini China, na kutoa mchango katika kuendeleza biashara huria na kudumisha utulivu wa mnyororo wa usambazaji duniani.

Pia wametoa maoni na mapendekezo juu ya kuendeleza uchumi wa mzunguko na wa kijani, kuboresha mazingira ya kufanyia biashara nchini China, na kuimarisha mawasiliano baina ya watu kati ya China na nchi za nje.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Li amesema anashukuru ushiriki wa wanunuzi hao wa muda mrefu katika maonyesho hayo, pamoja na ushirikiano wao mkubwa wa kiuchumi na kibiashara na China. Amebainisha kuwa kampuni nyingi za nchi za nje zimejenga uhusiano na China kupitia Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China, na zimekuwa imara sambamba na maendeleo ya China.

“Historia ya Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China ni historia ya kampuni kutoka duniani kote kuchangia fursa za China na kutimiza ushirikiano wa kunufaishana, na ni kielelezo cha ufunguaji mlango unaoendelea wa China katika soko la kimataifa,” Waziri Mkuu Li amesema.

Amesema China itafungua mlango wake zaidi kwa kiwango cha juu, na kuhimiza uwekezaji na biashara ziwe za huria na urahisi zaidi, amesema, akiongeza kuwa China itaendelea kuingiza utulivu katika biashara ya kimataifa na uchumi wa Dunia kwa uhakika wa maendeleo yake yenyewe, na kutoa nafasi pana kwa ajili ya maendeleo ya kampuni kutoka nchi mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha