Waziri Mkuu Netanyahu asema Israel inahifadhi haki yake ya kujilinda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock mjini Jerusalem, Aprili 17, 2024. (Maayan Toaf/GPO/ Xinhua)

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock mjini Jerusalem, Aprili 17, 2024. (Maayan Toaf/GPO/ Xinhua)

JERUSALEM - Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza "haki ya Israel ya kujilinda dhidi ya Iran," alipowapokea kwa nyakati tofauti Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock mjini Jerusalem.

Ziara hizo za mawaziri hao wawili wa mambo ya nje zimekuja wakati ambapo kuna shinikizo la kimataifa kwa Israel na Iran kupunguza hali ya wasiwasi kufuatia mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran kwa kutumia makombora na droni dhidi ya Israel mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwenye mikutano aliyofanya na mawaziri hao, Netanyahu amesisitiza kuwa "Israel inahifadhi haki yake ya kujilinda," kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, amesisitiza kuwa eneo hilo lazima liepuke mgogoro huo kupanuka. "Kila mtu lazima sasa atende kwa busara na kwa kuwajibika," amesema.

Kupanuka kwa mgogoro "hakutasaidia mtu yeyote," siyo usalama wa Israeli, au mateka ambao bado wanashikiliwa na Kundi la Hamas, mateso ya watu katika Ukanda wa Gaza, ya watu wengi nchini Iran, na ya nchi za tatu katika eneo hilo, amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Jerusalem, Cameron amesema anafanya ziara nchini Israel ili kuitaka ifanye "kidogo iwezekanavyo kuchochea mvutano" na kwa njia ambayo ni "ya busara na kali."

Kwenye hotuba yake katika kikao cha baraza la mawaziri baada ya mazungumzo na mawaziri hao wawili, Netanyahu amesema, "Mawaziri hao wawili wa mambo ya nje walikuwa na mapendekezo na ushauri mbalimbali. Ninashukuru. Lakini nataka kuweka wazi -- tutafanya maamuzi yetu wenyewe, na Israel itafanya kila linalohitajika kujilinda." 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Cameron mjini Jerusalem, Aprili 17, 2024. (Maayan Toaf/GPO/ Xinhua)

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Cameron mjini Jerusalem, Aprili 17, 2024. (Maayan Toaf/GPO/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha