Kampuni ya ujenzi ya China nchini Uganda yatoa mafunzo kwa wafanyakazi wenyeji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2024

Zhao Wei,  mwakilishi wa Shirika la Ujenzi wa Mawasiliano la China nchini Uganda, akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa "Mradi wa Mafunzo ya Vipaji wa Seagull" katika wilaya ya kati ya Wakiso, Uganda, Aprili 16, 2024. (Picha na John Tugume/Xinhua)

Zhao Wei, mwakilishi wa Shirika la Ujenzi wa Mawasiliano la China nchini Uganda, akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa "Mradi wa Mafunzo ya Vipaji wa Seagull" katika wilaya ya kati ya Wakiso, Uganda, Aprili 16, 2024. (Picha na John Tugume/Xinhua)

WAKISO, Uganda - Shirika la Ujenzi wa Mawasiliano la China (CCCC) limenza mafunzo ya wiki mbili siku ya Jumanne chini ya "Mradi wa Mafunzo ya Vipaji wa Seagull" kwa wasimamizi na wahandisi wenyeji katika wilaya ya katikati ya Uganda ya Wakiso ambayo yameandaliwa kwa msaada wa Chuo Kikuu cha Ufundi cha Wuhan katika Mkoa wa Hubei, China, na yanatarajiwa kutoa wakufunzi ambao watapitisha maarifa na ujuzi wao kwa wafunzwa 32.

Fan Xuecheng, konseli wa ubalozi wa China nchini Uganda, amesema elimu ya kazi za ufundi inasaidia watu kutumia ujuzi na vipaji vyao kuendeleza nchi yao, ambayo imekuwa muhimu kwa maendeleo ya China.

China iko tayari kunufaika na uzoefu wake pamoja na nchi za Afrika, Fan amesema kwenye hafla ya ufunguzi wa mradi huo wa kutoa mafunzo.

"Mafunzo ya kazi za ufundi na mawasiliano ya kitamaduni ni sehemu kubwa ya mawasiliano kati ya watu ya China na Uganda," amesema. "Tunapaswa kuungana mikono ili kuhakikisha maendeleo endelevu na kuwapa vijana wa Uganda hamasa za kujiendeleza zaidi baadaye ."

Esther Anyakun, Waziri wa Nchi wa Uganda anashughulikia kazi, ajira na uhusiano wa waajiri na waajiriwa , amesema mpango wa mafunzo kazi za ufundi ni muhimu katika maendeleo ya nchi, na kufungua uwezo wa watu binafsi.

Winfred Naluyinda, kamishna msaidizi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Uganda, amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati kwani nchi hiyo inatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi.

Zhao Wei, mwakilishi wa CCCC nchini Uganda, amesema tangu kuingia katika soko la Uganda Mwaka 1996, kampuni hiyo imefanikiwa kukamilisha miradi mingi, inayohusisha maelfu ya wafanyakazi wenyeji, wakiwa pamoja na wataalamu wa rasilimali watu, wahandisi wa tathmini ya mazingira, na wahandisi wa usalama hadi wasimamizi wa eneo la mradi na waendeshaji mashine.

"Watu wenyeji hao wenye ujuzi ni mali muhimu kwa kampuni," Zhao amesema.

Kwa mujibu wa kitabu cha mwongozo cha wanafunzi, program hiyo ya mafunzo itahusisha usanifu wa miradi ya uhandisi, mashine za ujenzi, na masomo ya lugha ya Kichina.

Mshiriki wa mafunzo akisoma vipeperushi kuhusu "Mradi wa Mafunzo ya Vipaji wa Seagull" kwenye hafla ya ufunguzi wa mradi huo katika wilaya ya kati ya Wakiso, Uganda, Aprili 16, 2024. (Picha na John Tugume/Xinhua)

Mshiriki wa mafunzo akisoma vipeperushi kuhusu "Mradi wa Mafunzo ya Vipaji wa Seagull" kwenye hafla ya ufunguzi wa mradi huo katika wilaya ya kati ya Wakiso, Uganda, Aprili 16, 2024. (Picha na John Tugume/Xinhua)

Esther Anyakun, Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia Kazi, Ajira na Uhusiano wa waajiri na waajiriwa , akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa "Mradi wa Mafunzo ya Vipaji wa Seagull" katika wilaya ya kati ya Wakiso, Uganda, Aprili 16, 2024. (Picha na John Tugume/Xinhua)

Esther Anyakun, Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia Kazi, Ajira na Uhusiano wa waajiri na waajiriwa, akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa "Mradi wa Mafunzo ya Vipaji wa Seagull" katika wilaya ya kati ya Wakiso, Uganda, Aprili 16, 2024. (Picha na John Tugume/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha