Mjumbe wa China ahimiza kuunga mkono matarajio ya Wapalestina ya utaifa na kujipatia uhuru

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 19, 2024

Fu Cong (Kati, mbele), mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, akizungumza kwenye mjadala wa wazi wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 18, 2024. (Xinhua/ Xie E)

Fu Cong (Kati, mbele), mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, akizungumza kwenye mjadala wa wazi wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 18, 2024. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Fu Cong, mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesema siku ya Alhamisi kwenye mjadala wa wazi wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina na Israel kwamba jumuiya ya kimataifa haipaswi kupuuza tena matarajio ya muda mrefu ya watu wa Palestina ya kutaka uhuru na kuanzisha nchi yao, wala kutowafanya waendelee kukumbwa na dhuluma za kihistoria.

Fu amesisitiza mahitaji ya dharura ya kutekeleza suluhu ya kuwepo kwa mataifa mawili.

"Suluhu ya mataifa mawili lazima itekelezwe kwa dhamira kubwa. Njia ya msingi ya kumaliza suala la Mashariki ya Kati iko katika utekelezaji wa suluhu ya mataifa mawili, ili Wapalestina na Waisraeli waweze kupata usalama wa pamoja na Waarabu na Wayahudi waweze kufikia maendeleo kwa pamoja," amesema Fu.

"Duru ya sasa ya mgogoro ni tahadhari ya majanga ya kutisha kwa jumuiya ya kimataifa kwamba haiwezi tena kukwepa matarajio ya watu wa Palestina ya kupata uhuru na kuanzisha nchi yao na kutowafanya waendelee kukumbwa na dhuluma ya kihistoria," ameongeza.

"Kwa upande huu, tunatoa wito wa kuitishwa kwa mkutano wa amani wa kimataifa ambao utakuwa na ushiriki mpana na ufanisi zaidi ili kuandaa ratiba na dira ya utekelezaji wa suluhu ya mataifa mawili," ameongeza.

Baraza la Usalama lilikuwa likitazamiwa kupiga kura baadaye siku hiyo ya Alhamisi juu ya ombi la Palestina la kuwa nchi mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa.

Balozi Fu amesisitiza umuhimu wa uungaji mkono wa kimataifa wa mara moja kwa ombi jipya la Palestina la kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa, akizitaka nchi wanachama wote wa baraza hilo kupiga kura ya ndiyo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha