Marekani yapiga kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama kupinga ombi la Palestina la kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 19, 2024

Naibu Mjumbe wa Kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Robert Wood (Kulia mbele) akipiga kura dhidi ya mswada wa azimio linalopendekeza kwa nchi wanachama 193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba "Nchi ya Palestina ikubaliwe uanachama wa Umoja wa Mataifa" katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, tarehe 18 Aprili 2024. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Marekani imepiga kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama kupinga ombi la Palestina kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa wakati baraza hilo lenye nchi wanachama 15 lilipopigia kura mswada wa azimio linalopendekeza kwa nchi wanachama 193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba "Palestina likubaliwe kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa."

Mswada huo umepata kura 12 za ndiyo, mbili hazikushiriki, na kura moja ya kupinga.

Mswada huo unahitaji angalau kura tisa za kuunga mkono na kutokuwepo kwa kura yoyote ya turufu kutoka nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia au China ili kupitishwa. Marekani imelazimika kutumia kura yake hiyo ya turufu baada ya mswada huo kupata kura 12 za ndiyo.

Ujumbe wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa hapo awali uliomba hadhi ya kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa Mwaka 2011. Jaribio lao la kwanza lilishindwa kwa sababu halikupata uungwaji mkono wa chini unaohitajika wa nchi wanachama tisa kati ya 15 wa Baraza la Usalama.

Baada ya kushindwa kwao huko kwa mara ya kwanza, Wapalestina walifanikiwa kupandisha hadhi yao kutoka "mwangalizi wa Umoja wa Mataifa" hadi "nchi mwangalizi isiyo mwanachama" kwa kupata theluthi zaidi ya mbili ya kura katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika Mwezi Novemba Mwaka 2012.

Kupandishwa huko kwa hadhi kuliwezesha Palestina kujiunga na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na ya kimataifa, kama vile Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Siku hiyo ya Alhamisi, Ziad Abu Amr, mjumbe maalum wa Rais wa Palestina, alihutubia Baraza la Usalama, na kusema kwamba kupitishwa kwa azimio hilo kutawapa watu wa Palestina matumaini ya "maisha ya heshima ndani ya nchi huru."

Wajumbe wakipiga kura juu ya mswada wa azimio linalopendekeza kwa nchi wanachama 193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba "Nchi ya Palestina ikubaliwe uanachama wa Umoja wa Mataifa", katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, tarehe 18 Aprili 2024. (Xinhua/Xie E)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha