Lugha Nyingine
Rais Xi akabidhi bendera kwa kikosi cha uungaji mkono wa upelekaji wa habari cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA)
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza kwenye hafla ya kuanzishwa kwa kikosi cha uungaji mkono wa upelekaji wa habari cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) mjini Beijing, China, Aprili 19, 2024. (Xinhua/Li Gang)
BEIJING - Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) limeanzisha kikosi cha uungaji mkono wa upelekaji wa habari ambapo Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amewasilisha bendera kwa kikosi hicho katika hafla ya kuanzishwa kwake iliyofanyika siku ya Ijumaa mjini Beijing.
Kwenye hafla hiyo, Rais Xi amesisitiza juhudi madhubuti za kujenga kikosi imara na chenye maendeleo ya mambo ya kisasa cha uungaji mkono wa upelekaji wa habari.
Amesema kuwa kuanzishwa kwa kikosi hicho ni uamuzi mkubwa wa Kamati Kuu ya Chama na Kamati Kuu ya Kijeshi kutokana na kuimarisha mambo ya jumla ya kujenga jeshi lenye nguvu.
Amesisitiza kuwa kikosi hicho ni kikosi cha aina mpya cha kimkakati cha jeshi na ni nguzo muhimu katika kufanya mpango wa jumla wa ujenzi na matumizi ya mfumo wa upashanaji wa habari za mtandao, kikosi hicho kitakuwa na nafasi muhimu na kubeba jukumu kubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya kiwanda cha juu ya jeshi la China chenye uwezo wa kupata ushindi katika vita vya kisasa.
Amesisitiza kuwa, kikosi hicho kinapaswa kutii kwa uthabiti amri ya Chama, na ni lazima kuhakikisha kikosi hicho kuwa mwaminifu, msafi na cha kutegemewa daima.
Rais Xi amehimiza kikosi hicho kufungamana kwa kina katika mfumo wa operesheni ya pamoja ya jeshi la China, kutoa uungaji mkono wa upelekaji wa habari kwa usahihi na ufanisi, na kutoa huduma za uhakikisho kwa operesheni za kijeshi katika pande mbalimbali na nyanja mbalimbali.
Pia amehimiza juhudi za kuimarisha mfumo wa habari za mtandaoni unaokidhi matakwa ya vita vya kisasa, na unaoonesha umaalum wa jeshi la China, ili kuhimiza uwezo wa kufanya vita kwenye mfumo kamili kwa sifa bora na ufanisi zaidi.
Rais Xi alikutana na wajumbe wa uongozi wa kikosi hicho cha uungaji mkono wa upelekaji wa habari na kupiga picha pamoja nao.
Kwa mujibu wa uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, kikosi hicho kinaongozwa moja kwa moja na Kamati Kuu ya Kijeshi, na nambari ya Kikosi cha Uungaji mkono wa Kimkakati imefutwa, hivyo utarekebishwa kwa uhusiano wa uongozi na usimamizi kati ya vikosi vilivyohusika.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikabidhi bendera kwa kikosi cha uungaji wa mkono wa upelekaji wa habari cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kwenye hafla ya kuanzishwa kwake mjini Beijing, China, Aprili 19, 2024. (Xinhua/Li Gang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma