China yaandaa Kongamano la 19 la Vikosi vya Wanajeshi wa Majini vya Eneo la Pasifiki Magharibi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2024

Bendi ya jeshi ikitumbuiza kwenye Jumba la Makumbusho ya Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) kusherehekea maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha China huko Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Aprili 20, 2024. (Xinhua/Li Ziheng)

Bendi ya jeshi ikitumbuiza kwenye Jumba la Makumbusho ya Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) kusherehekea maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha China huko Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Aprili 20, 2024. (Xinhua/Li Ziheng)

QINGDAO - Mkutano wa 19 wa Kongamano la Vikosi vya Wanajeshi wa Majini vya Eneo la Pasifiki Magharibi (WPNS) wenye kaulimbiu ya "Bahari za Mustakabali wa Pamoja wa Siku za Baadaye", umefunguliwa Jumapili katika mji wa bandari wa Qingdao katika Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. Mkutano huo wa siku nne unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 180 wa vikosi vya wanajeshi wa majini kutoka nchi 29, zikiwemo Australia, Cambodia, Chile, Ufaransa na India.

Wajumbe kwenye mkutano huo watafanya mapitio ya shughuli zinazofanyika chini ya mfumo wa kongamano hilo tangu mkutano wake wa 18, kuweka ajenda za siku za baadaye, na kujadili na kupiga kura kuhusu masuala kama vile Mkataba wa shughuli za WPNS, Kanuni za Kukutana Kusikotarajiwa Baharini (CUES), na mfumo usioendeshwa na binadamu.

Viongozi wa kigeni wa vikosi hivyo vya majini wataalikwa kujadili Pendekezo la Usalama wa Dunia na amani ya baharini, utaratibu wa baharini unaozingatia ushirikiano wa usalama wa baharini na sheria za kimataifa, na usimamizi wa kimataifa wa baharini.

Liang Wei, afisa mwandamizi wa Chuo cha Utafiti wa Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha China (NRA), amesema ushiriki katika mkutano huo na ngazi za maafisa wanaoshiriki kutoka nchi nyingine ni za juu.

"Hii siyo tu inaonyesha nguvu ya kongamano lakini pia inaonyesha ushawishi na mvuto wa kikosi cha wanajeshi wa majini cha China," Liang amesema.

Ikiwa ni mwanachama mwanzilishi wa WPNS, China iliandaa kwa mara ya kwanza mkutano wa 14 wa WPNS huko Qingdao Mwaka 2014. Katika mkutano huo, nchi wanachama ziliidhinisha Kanuni za Kukutana Kusikotarajiwa Baharini CUES, mfumo wa kati ya vikosi vya wanajeshi wa majini ulioundwa ili kupunguza kutoelewana na kuepuka ajali za baharini.

Kwa sasa, WPNS ina nchi wanachama 23 na nchi saba waangalizi. Kongamano hilo hufanya mikutano na lina miradi ya mawasiliano kwa maofisa vijana wa kijeshi ikiwa ni pamoja na masajenti waandamizi na wachanga.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha