Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Papua New Guinea wafanya mazungumzo na kufikia makubaliano juu ya uhusiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Papua New Guinea Justin Tkatchenko wakifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao huko Port Moresby, Papua New Guinea, Aprili 20, 2024. (Xinhua/Ma Ping)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Papua New Guinea Justin Tkatchenko wakifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao huko Port Moresby, Papua New Guinea, Aprili 20, 2024. (Xinhua/Ma Ping)

PORT MORESBY - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) alisema siku ya Jumamosi kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Papua New Guinea (PNG) Justin Tkachenko kuwa amekuwa na mazungumzo ya kina na ya kirafiki na Tkachenko huku makubaliano mapana yakiwa yamefikiwa kuhusu uhusiano wa pande mbili.

Wang na Tkachenko wanakubaliana kuwa China na Papua New Guinea zinapaswa kuendelea kuaminiana na kuungana mkono, na kudumisha na kuendeleza bila kuyumba yumba ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

Wang amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Papua New Guinea, China siku zote imekuwa ikiichukulia nchi hiyo kama mwenzi muhimu na rafiki wa karibu, inauchukua uhusiano wa pande hizo mbili kwa mtazamo wa kimkakati na kuimarisha mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwa usawa.

“China inaunga mkono kithabiti PNG katika kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi yake, ikiwa ni pamoja na kufuata njia ya mafanikio ya maendeleo inayoendana na hali yake halisi ya kitaifa” amesema Wang, huku pia akipongeza PNG kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kuunga mkono maslahi ya msingi na masuala makuu yanayofuatiliwa na China.

Wang na Tkachenko wamekubaliana kwa kauli moja kujikita katika maendeleo kila wakati, kutilia maanani ustawi wa watu, na kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja zote.

Wang amesema kuwa PNG ilikuwa nchi ya kwanza ya visiwa vya Pasifiki kutia saini nyaraka za makubaliano na mpango wa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na imekuwa mwenzi mkubwa wa kibiashara, eneo linalowekezwa zaidi na China na soko la ujenzi wa miundombinu la China katika eneo hilo.

Wang na Tkachenko pia wametetea kwa kauli moja kwamba masuala ya ndani ya nchi za visiwa vya Pasifiki yasiingiliwe, haki yao ya kujiendeleza kwa kujitegemea isinyimwe, na mazingira ya amani na utulivu lazima yalindwe.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha