Mjumbe wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuimarishwa kwa usalama nchini Haiti ili kuhimiza maendeleo ya kisiasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano kuhusu hali ya Haiti kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 22, 2024. (Manuel Elias/Picha ya Umoja wa Mataifa/ Xinhua)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mkutano kuhusu hali ya Haiti kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 22, 2024. (Manuel Elias/Picha ya Umoja wa Mataifa/ Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Maria Isabel Salvador, mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Haiti siku ya Jumatatu kwenye mkutano wa Baraza la Usalama amesisitiza haja ya kuimarishwa kwa usalama nchini Haiti ili kupata maendeleo zaidi ya kisiasa huku pia akipongeza maendeleo ya hivi majuzi ya kisiasa nchini humo, hasa kuanzishwa kwa Baraza la Mpito la Urais(TPC).

"Ninawaomba wadau wote wa Haiti kuweka mipango ya utawala wa mpito haraka iwezekanavyo, hasa uteuzi wa waziri mkuu na serikali ya mpito, na uteuzi wa haraka wa Baraza la Mpito la Uchaguzi," amesema.

Hata hivyo, amesema kuimarishwa kwa usalama ni sharti la muhimu kwa maendeleo zaidi ya kisiasa.

Licha ya maendeleo mazuri ya hivi majuzi katika upande wa kisiasa, hali ya usalama iliyoimarishwa zaidi inaendelea kuwa jambo la muhimu kwa maendeleo zaidi. Viongozi wa magenge na waharibifu wengine wameeleza nia yao ya kuvuruga kwa mabavu mchakato wa sasa wa kisiasa, amesema. "Napaswa kusisitiza hitaji la kuisaidia Haiti katika juhudi zake za kurejesha usalama", ameongeza.

Salvador ametoa wito wa kutumwa haraka kwa tume ya Kimataifa ya Usalama, ambao uliidhinishwa na Baraza la Usalama Oktoba 2023.

Ameongeza kuwa, vikwazo vilivyowekwa dhidi ya makundi ya magenge ya Haiti ni chombo madhubuti cha kuzuia majaribio ya waharibifu wa amani na wahalifu, kuelekea maendeleo ya uwazi ya kisiasa na demokrasia.

Wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya 2024, watu karibu 2,500 waliuawa au kujeruhiwa kutokana na ghasia za magenge, ikifanya kipindi hiki kuwa chenye vurugu zaidi tangu kitengo cha haki za binadamu cha BINUH kianze kurekodi takwimu Januari 2022, amesema.

Amesema, mpango wa mwitikio wa misaada ya kibinadamu kwa Haiti kwa Mwaka 2024, ambao unahitaji dola za Marekani milioni 674, unafadhiliwa kwa asilimia 8.1 pekee. “Bado hali ya kibinadamu inaendelea kuongezeka kuwa mbaya,” amesema.

Maria Isabel Salvador (kwenye skrini), mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, akizungumza kwa njia ya video katika mkutano wa Baraza la Usalama, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 22, 2024. (Eskinder Debebe/Picha ya UN / Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha