Siku ya Lugha ya Kichina yaadhimishwa kwenye Umoja wa Mataifa kwa maonyesho ya utamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2024
Siku ya Lugha ya Kichina yaadhimishwa kwenye Umoja wa Mataifa kwa maonyesho ya utamaduni
Wageni wakipiga picha kwenye maonyesho ya utamaduni wa China kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifakwenye makao makuu ya Umoja huo, Aprili 19, 2024. (Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA – Lugha ya Kichina, mojawapo ya lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa (UN) na inayotumiwa na watu wanaokaribia theluthi moja duniani kote, ni sehemu muhimu ya urithi wa utamaduni wa binadamu, Denis Francis, Rais wa mkutano wa Baraza Kuu la 78 la Umoja wa Mataifa, amesema siku Ijumaa kwenye maonyesho ya utamaduni wa China katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Maonyesho hayo yenye kaulimbiu ya "Kukutana na Maandishi ya Lugha ya Kichina, Mapatano na Kuishi pamoja," yameandaliwa na Mji wa Nanjing, mji mkuu wa Mkoa wa Jiangsu wa China, kuadhimisha Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Maonyesho hayo yametoa mchangamano wa kina wa uelewa wa utamaduni ambao umejumuisha maandishi ya Lugha ya Kichina, uchoraji, muziki na chai.

Lugha siyo tu njia ya mawasiliano bali pia ni daraja linalounganisha watu na tamaduni mbalimbali, na hivyo kuboresha uzoefu wetu wa maisha, amesema Francis, ambaye alishiriki katika kazi ya kuandika maandishi ya Kichina.

"Katika ziara yangu nchini China Januari mwaka huu, nilipata fursa ya kujaribu sanaa ya maandishi ya Kichina. Niliandika herufi ya Kichina 'Fu,' ikimaanisha 'furaha,’" amesema.

Siku za Lugha za Umoja wa Mataifa, zilizoanza kuadhimishwa rasmi Mwaka 2010, husherehekea uwepo wa lugha mbalimbali tofauti na uanuai wa utamaduni duniani na kuendeleza matumizi sawa ya lugha sita rasmi za umoja huo: Kiarabu, Kichina, Kiingereza, Kifaransa, Kirusi na Kihispania.

Tarehe ya Siku ya Lugha ya Kichina mbayo huangukia Aprili 20 kila mwaka, ilichaguliwa kutoka Guyu, au Mvua ya Nafaka, mzunguko wa sita kati ya siku 24 ya hali ya hewa katika kalenda ya kilimo ya China, ili kukumbuka Cangjie, mtu mashuhuri katika China ya kale anayetambuliwa kuwa mvumbuzi wa maandishi ya Lugha ya Kichina.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha