Waziri Mkuu wa Uingereza asema wahamiaji nchini humo wataanza kupelekwa Rwanda ndani ya miezi mitatu

(CRI Online) April 23, 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amesema, makubaliano ya kuhamisha wahamiaji kati ya nchi hiyo na Rwanda yataanza kutekelezwa ndani ya kipindi cha wiki 10 hadi 12 zijazo ambapo ndege ya kwanza itakayokuwa imebeba wahamiaji hao itaondoka Uingereza kuelekea Rwanda.

Hayo yamekuja wakati baadaye siku hiyo Bunge la Uingereza lilipitisha mswada ambao ulikuwa umekwama kwa muda mrefu bungeni wa kuipa idhini serikali ya Uingereza kuhamisha wahamiaji nchini Rwanda.

Makubaliano hayo yaliyosainiwa mwezi Desemba mwaka jana mjini Kigali, Rwanda, na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili, yalikuwa yanalenga kukwamua Ushirikiano wa Uhamiaji na Maendeleo ya Kichumi wa Uingereza na Rwanda (MEDP), ambao ulipingwa na Mahakama Kuu ya Uingereza mwezi Novemba mwaka jana.

Waziri Mkuu, Sunak aliwasilisha bungeni mswada uliolenga kukwamua ushirikiano huo kutoka kwenye kikwazo cha mahama, ambao bunge limeupitisha.

Utaratibu huo unalenga kuwahamisha watu walioingia Uingereza kwa kutumia boti ndogo na kuwapeleka Rwanda ambako wataweza kuomba hifadhi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha