Rais wa Kenya atoa wito wa kuoanishwa kwa sera za TEHAMA kote barani Afrika

(CRI Online) April 23, 2024

Rais wa Kenya William Ruto ametoa wito wa kuoanishwa kwa sera za teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kote barani Afrika siku ya Jumatatu ili kuchochea mageuzi ya kidijitali.

Rais Ruto ameyasema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa “Afrika iliyounganishwa wa 2024”, ulioanza mjini Nairobi, nchini Kenya.

Amefafanua kuwa ushirikiano huo unapaswa kuongozwa na mtandao wa mamlaka za TEHAMA na kusimamiwa na ujumuishaji wa mipango ya mageuzi ya kidijitali.

Rais Ruto amesema kuwa kuoanisha sera za kidijitali katika bara zima kutasaidia kuharakisha azma ya Afrika kujiweka mbele kabisa kwenye biashara ya kimataifa, hasa kwenye utekelezaji wa makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha