Nchi za Asia-Pasifiki zatoa mwito wa kukumbatia fursa za kidijitali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2024

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu akitoa hotuba kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 80 wa Kamisheni ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Asia na Pasifiki (ESCAP) mjini Bangkok, Thailand, Aprili 22, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

BANGKOK - Viongozi wa serikali na watunga sera kutoka nchi za Eneo la Asia-Pasifiki wamekusanyika Bangkok, Thailand kuanzia siku ya Jumatatu wakitoa mwito wa kukumbatia fursa za kidijitali na kutumia kikamilifu fursa za teknolojia na uvumbuzi wa kidijitali unaoibukia kwa maendeleo endelevu.

Mawaziri wakuu wa Thailand na Cambodia, na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu ni miongoni mwa washiriki wapatao 800 wa Mkutano wa 80 wa Kamisheni ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Asia na Pasifiki (ESCAP) ulioitishwa kujadili njia za kidijitali ili kuharakisha maendeleo endelevu ya eneo hilo.

"Suluhu za kidijitali zinazotumika kwa umakini na kusimamiwa ipasavyo, juu ya msingi wa uelewa wa pamoja, mbinu za pamoja na usimamizi shirikishi, zinaweka misingi ya msukumo wa pamoja unaohitajika kwa ajili ya kufikia Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu," Armida Salsiah Alisjahbana, Katibu Mtendaji wa ESCAP, amesema katika hotuba yake ya ufunguzi.

Waziri Mkuu wa Thailand Srettha Thavisin amebainisha kuwa kwa nchi nyingi za eneo la Asia-Pasifiki zinazotegemea kilimo, ikiwa ni pamoja na Thailand, mageuzi ya kidijitali ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa chakula kwa wote.

"Tunahitaji kutumia teknolojia za kidijitali ipasavyo kukuza uvumbuzi wa kilimo. Hii itasaidia kuhakikisha mfumo endelevu wa chakula, kilimo cha kisasa kinachotilia maanani mabadiliko ya tabianchi, na uendelevu wa mazingira," ameongeza.

Katika hotuba yake kwenye mjadala mkuu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Ma Zhaoxu, amebainisha kuwa, katika kukabiliana na hali ngumu, pande zote zinapaswa kutumia ushirikiano wa pande nyingi, kuhimiza dunia ya pande nyingi zenye uwiano wa nguvu yenye usawa na utaratibu na utandawazi jumuishi wa uchumi, na kushirikiana ili kujenga Jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya Asia na Pasifiki.

Washiriki katika mkutano huo wamejadili jinsi ya kunufaika kikamilifu na uvumbuzi wa kidijitali huku wakijilinda dhidi ya hatari zinazoweza kutokea, wakitoa wito wa kutekeleza sera jumuishi ili kupunguza pengo la kidijitali na ukosefu wa usawa unaoendelea, kushughulikia ipasavyo masuala kama vile usalama wa mtandao na faragha ya data, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda ili kuhakikisha kwamba uvumbuzi wa kidijitali unanufaisha wote.

Ukiwa utafanyika kuanzia Aprili 22 hadi 26, mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu ya Kutumia kikamilifu Uvumbuzi wa Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu ya Eneo la Asia-Pasifiki.

ESCAP, iliyoanzishwa mwaka 1947, ni tawi la maendeleo ya kikanda la Umoja wa Mataifa katika eneo la Asia-Pasifiki, ikiwakilisha asilimia zaidi ya 60 ya watu duniani.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu akitoa hotuba kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 80 wa Kamisheni ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Asia na Pasifiki (ESCAP) mjini Bangkok, Thailand, Aprili 22, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu akitoa hotuba kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 80 wa Kamisheni ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Asia na Pasifiki (ESCAP) mjini Bangkok, Thailand, Aprili 22, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu akitoa hotuba kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 80 wa Kamisheni ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Asia na Pasifiki (ESCAP) mjini Bangkok, Thailand, Aprili 22, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Ma Zhaoxu akitoa hotuba kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 80 wa Kamisheni ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Asia na Pasifiki (ESCAP) mjini Bangkok, Thailand, Aprili 22, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha