Marekani kuanza uchunguzi dhidi ya magari yanayotumia umeme ya China

(CRI Online) April 24, 2024

Serikali ya Marekani imetangaza kuwa itaanza uchunguzi dhidi ya magari yanayotumia umeme yaliyozalishwa China kwa kile ilichodai ni “tishio la usalama wa taifa”, ikiwa ni muda mfupi baada ya kampuni ya magari yanayotumia umeme ya BYD ya China kutangaza mpango wa kujenga kiwanda nchini Mexico.

Akizungumzia suala hilo, aliyekuwa mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani, Prof. John Quelch amesema, magari yanayotumia umeme ya China mpaka sasa hayapo kwenye soko la Marekani, lakini kama kampuni ya China ikianza kuzalisha magari nchini Mexico, huenda magari hayo yataingia kwenye soko la Marekani.

Ameongeza kuwa, kwa upande wa China, hatua hiyo ni nzuri, lakini kwa upande wa Marekani, sekta yake ya magari imehisi tishio, na kuchukua hatua ya kujilinda.

Hata hivyo, kampuni kubwa za magari duniani zimeeleza nia ya kuongeza uwekezaji na kuharakisha mageuzi ili kukidhi mahitaji kwenye soko la China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha