Mazungumzo mapya ya Marekani kuhusu kile inachokiita“Uzalishaji bidhaa wa China kuliko uwezo wa soko” yatafanikiwa?

(CRI Online) April 24, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara yake ya pili nchini China kuanzia leo Jumatano, tarehe 24 April.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi za nje, Bw. Blinken atafuata hatua za Waziri wa Fedha Janet Yellen, na kuendelea kuzungumzia kile kinachoitwa “ Uzalishaji bidhaa wa China kuliko uwezo wa soko”.

Bibi Yellen alipozungumzia suala hili wakati ziara yake ya hivi karibuni nchini China alisema, uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya China, hususan vya magari yanayotumia nishati mpya umezidi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya soko la ndani la China, na pia umezidi yale ya soko la kimataifa, hali ambayo itaweza kusababisha bidhaa kuuzwa kwa bei ya chini, na kuleta athari mbaya kwa kampuni na wafanyakazi nchini Marekani na nchi nyingine.

Lakini baadhi ya wachambuzi wa uchumi nchini Marekani hawakubaliani na kauli hii ya Bibi Yellen, kwani inakwenda kinyume na kanuni za msingi za uchumi wa soko huria ambazo nchi za Magharibi zimekuwa zikizitetea kwa zaidi ya miaka 200.

Imeonekana kuwa viwanda ambavyo China ina uwezo mkubwa zaidi wa kiushindani ikilinganishwa na Marekani, ndivyo vinatajwa na Marekani kuwa “viwanda vyenye uzalishaji mkubwa wa bidhaa kuliko uwezo wa soko”.

Madhumuni ya hatua hiyo ya ujanja ya Marekani ni kushusha hadhi ya viwanda hivyo vya China kwa kile inachodai kuwa ni “tishio”, ili kuzuia maendeleo ya viwanda hivyo.

Lakini ukweli ni kuwa, uzalishaji wa magari yanayotumia nishati mpya wa China hauzidi uwezo na mahitaji ya soko, bali bado kuna safari ndefu ya kukua, na ili kufikia lengo la kuondoa hewa chafu duniani, bado inahitajika uwezo mkubwa zaidi wa magari ya nishati mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha