Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China akanusha shutuma za nchi za magharibi za "Uzalishaji kupita mahitaji ya soko"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2024

BEIJING - Baadhi ya nchi za Magharibi hivi majuzi zimekuwa zikiishutumu China kwa "Uzalishaji kupita mahitaji ya soko," shutuma ambazo ni kelele isiyo na msingi na China inazipinga kithabiti, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wang Wenbin amesema siku ya Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa G7 ulitoa taarifa hivi karibuni, ukidai kwamba sera ya China siyo ya soko huria na vitendo vya China vinasababisha "uzalishaji bidhaa kupita mahitaji ya soko."

Alipoulizwa kwenye mkutano huo na waandishi wa habari na kutakiwa kutoa maoni yake juu ya tamko hilo, Wang alisema kwamba uwezo wa sekta ya nishati mpya ya China ni wa kiwango cha juu na unaohitajika sana kwa maendeleo ya kijani, na siyo "uzalishaji bidhaa kupita mahitaji ya soko."

Amesema, teknolojia na bidhaa za kijani za China, hususan ukuaji wa sekta ya nishati mpya, unakidhi mahitaji ya nchi kushughulikia msukosuko wa nishati na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na utatoa mchango muhimu kwa ajili ya dunia nzima kubadilisha muundo wa uzalishaji bila uchafuzi na kutoa kaboni chache.

Wang amesema, “Ukuaji wa kasi wa viwanda vya uzalishaji bidhaa za nishati mpya vya China unalingana na kanuni za uchumi na kanuni za soko, siyo matokeo ya kupata ruzuku,” na viwanda vya uzalishaji bidhaa za nishati mpya vya China ni vyenye nguvu bora ya kiteknolojia, kwa sababu vilianza mapema na vilifanyiwa utafiti wa maendeleo na kupata uwekezaji kwa muda mrefu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha