China yatangaza jukumu la safari ya anga ya juu ya chombo cha Shenzhou-18 kinachowabeba wanaanga

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2024

Picha hii isiyo na tarehe ikiwaonyesha wanaanga wa China Ye Guangfu (Kati), Li Cong (Kulia) na Li Guangsu ambao  watatekeleza jukumu la safari kwenye anga ya juu ya chombo cha Shenzhou-18. (Xinhua)

Picha hii isiyo na tarehe ikiwaonyesha wanaanga wa China Ye Guangfu (Kati), Li Cong (Kulia) na Li Guangsu ambao watatekeleza jukumu la safari kwenye anga ya juu ya chombo cha Shenzhou-18. (Xinhua)

JIUQUAN - Wanaanga wa China Ye Guangfu, Li Cong na Li Guangsu watatekeleza jukumu la safari kwenye anga ya juu ya chombo cha Shenzhou-18, na Ye atakuwa kiongozi wa jukumu hilo, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limetangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku ya Jumatano.

Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-18 kinatarajiwa kurushwa baadaye leo Alhamisi majira ya saa 2:59 (Kwa saa za Beijing) kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China, amesema Lin Xiqiang, naibu mkurugenzi wa CMSA.

Baada ya kuingia kwenye obiti, chombo hicho cha anga ya juu cha Shenzhou-18 kitafanya minyumbuliko ya kiotomatiki ya haraka na kutua kwenye eneo la moduli ya msingi ya kituo cha Tianhe cha anga ya juu cha China, ambapo muda huu utachukua masaa takriban 6.5, na kuunda mchanganyiko wa moduli tatu na vyombo vitatu vya anga ya juu, Lin amesema.

Hii itakuwa ni safari ya pili kwenye anga ya juu kwa mwanaanga Ye Guangfu ambaye alikuwa pia ni mwanaanga aliyetekeleza jukumu la safari kwenye anga ya juu ya chombo cha Shenzhou-13 kuanzia Oktoba 2021 hadi Aprili 2022. Li Cong na Li Guangsu, ambao ni miongoni mwa kundi la tatu la kizazi cha wanaanga wa China, wote ni wapya kwenye safari za chombo kwenye anga ya juu.

Ye Guangfu (Kati), Li Cong (Kulia) na Li Guangsu, wanaanga watatu wa China watakaotekeleza jukumu la safari kwenye anga ya juu ya  chombo cha Shenzhou-18, wakikutana na waandishi wa habari kwenye Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, Aprili 24, 2024. (Xinhua/Bei Yeye)

Lin amesema, wanaanga hao watakaa kwenye obiti kwa miezi takriban sita, na watashuhudia kuwasili kwa chombo cha mizigo cha Tianzhou-8 na chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-19 wakati wa kuwepo kwao huko.

Picha hii iliyopigwa Aprili 17, 2024 ikionyesha muunganisho wa chombo cha safari kwenye anga ya juu cha Shenzhou-18 na roketi ya ya Long March-2F kwa pamoja vikihamishwa hadi eneo la kurushia vyombo kwenda anga ya juu la Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Aprili 17, 2024 ikionyesha muunganisho wa chombo cha safari kwenye anga ya juu cha Shenzhou-18 na roketi ya Long March-2F kwa pamoja vikihamishwa hadi eneo la kurushia vyombo kwenda anga ya juu la Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha