Teknolojia ya AR yafanya mabaki ya kale katika Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu “yajongee”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2024

Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu, ambayo yameorodheshwa kwenye Urithi wa Kitamaduni wa Dunia na “ushahidi wa historia ya miaka 5,000 ya ustaarabu wa China”, ni makumbusho ya kwanza duniani kutumia teknolojia ya AR katika kufahamisha utangulizi watembeleaji. Tarehe 22, Aprili, mwandishi wa habari wa People’s Daily Online alivaa miwani ya AR ya kufanya utangulizi na alikuwa na umbali wa mguso wa karibu na ustaarabu wa Liangzhu: ramani ya makumbusho hayo ilijionyesha mbele ya macho yake, na mabaki ya kitamaduni kama vile vyungu vya udongo vyenye alama za kuchongwa, na hazina za kale nyinginezo za thamani zilijitokeza kwenye kiganja cha mikono yake…… Ikichanganya teknolojia za utambuzi wa picha na sauti, na nyinginezo, Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu hutumia miwani ya AR “kufufusha” mabaki hayo ya kale, na kutoa huduma ya maelezo inayoonekana kwa watembeleaji wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha