Kutazama Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu ndani ya sekunde 30

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2024

Tarehe 22, Aprili, timu ya waandishi wa habari wa People's Daily Online ya “Kutazama China” iliingia Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu kutembelea mabaki ya kale ya makumbusho hayo na kuhisi umuhimu wa ustaarabu wa Liangzhu katika kipindi cha kuanza kwa ustaarabu wa China.

Makumbusho hayo yapo kwenye eneo la Yuhang la Mji wa Hangzhou, China. Ni makumbusho ya eneo la kiakiolojia linalohusisha kazi za kuhifadhi, kufanya utafiti, kuonesha na kueneza utamaduni wa Liangzhu. Utafiti wa kiakiolojia unaonesha kuwa, ustaarabu wa Liangzhu ulikuwepo kati ya miaka 5,300 hadi 4,300 iliyopita. Neno “Liangzhu”katika Lugha ya Kichina linamaanisha “ardhi nzuri katikati ya maji”. Magofu ya ustaarabu wa Liangzhu ni sehemu takatifu inayothibitisha historia ya miaka 5,000 ya ustaarabu wa China, na yameorodheshwa kwenye orodha ya urithi wa dunia tarehe 6, Julai, 2019.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha