Russia yapiga kura ya turufu dhidi ya mswada wa azimio la Baraza la Usalama kuhusu silaha za maangamizi katika anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2024

Wajumbe wakipigia kura mswada wa azimio kuhusu kuwekwa kwa silaha za maangamizi katika anga ya juu kwenye mkutano wa Baraza la Usalama katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 24, 2024. (Loey Felipe/UN/Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA – Russia imepiga kura ya turufu siku ya Jumatano dhidi ya mswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuwekwa kwa silaha za maangamizi katika anga ya juu iliyowasilishwa na Marekani na Japan na kupata uungwaji mkono wa nchi wajumbe 13 kati ya 15 wa Baraza la Usalama. Russia, ambayo ina haki ya kura ya turufu, ilipiga kura kupinga mswada huo. China haikupiga kura.

Kabla ya kupiga kura hiyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikataa marekebisho ya mswada wa azimio hilo yaliyopendekezwa na Russia na China ili kujumuisha kipengele cha kupiga marufuku kuweka silaha katika anga ya juu.

Mjumbe wa kudumu wa Russia kwenye Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia, amezishutumu Marekani na Japan kwa kufanya "onyesho chafu" katika Baraza la Usalama kwa kuwasilisha mswada huo.

"Kwa mwonekani wa kwanza, inaonekana haina madhara, inaonekana chanya, kwa sababu inajikita rasmi kwa mada ambayo ni ya muhimu sana kwa jumuiya ya kimataifa -- hiyo ni kutoweka kwa WMD (silaha za maangamizi) katika anga ya juu.

Hata hivyo nyuma ya nia hii njema, kuna mpango wa hila ambao umetungwa na wenzetu wa Magharibi," ameliambia baraza hilo kabla ya kupiga kura.

Nebenzia ameeleza kuwa marufuku ya kuweka silaha za maangamizi WMDs katika anga ya juu tayari imeingizwa kwenye Mkataba wa Anga ya Juu wa 1967. Marekani na Japan zilikuwa na nia fiche ya kuchagua WMDs kutoka kwenye aina nyingine zote za silaha katika anga ya juu.

Kwa kufanya hivyo, Marekani na Japan zinaweza kufichua nia yao ya kutokuwa na ufuatiliaji kwa anga ya juu isiyo na silaha zozote, alisema.

Wajumbe wakipigia kura mswada wa azimio kuhusu kuwekwa kwa silaha za maangamizi katika anga ya juu kwenye mkutano wa Baraza la Usalama katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 24, 2024. (Loey Felipe/UN/Xinhua)

Wajumbe wakipigia kura mswada wa azimio kuhusu kuwekwa kwa silaha za maangamizi katika anga ya juu kwenye mkutano wa Baraza la Usalama katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Aprili 24, 2024. (Loey Felipe/UN/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha