Kauli ya "Kuuza Bidhaa nyingi Nje ni sawa na Uwezo wa ziada wa uzalishaji" Haina msingi wowote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2024

Magari yanayotumia nishati mpya, betri za lithiamu, na bidhaa za kuzalisha umeme kwa nishati ya jua. Mwaka jana, thamani ya mauzo ya nje ya bidhaa hizo tatu mpya za China kwa mara ya kwanza ilizidi Yuan trilioni moja, ikiwa ni ongezeko la karibu asilimia 30. Watu wengi katika sekta ya uchumi wa kimataifa wameipongeza China kwa uhamasishaji wake thabiti wa mageuzi ya kijani.

Hata hivyo, baadhi ya watu nchini Marekani wameipa jina sekta ya nishati mpya ya China kuwa ni “Uwezo wa ziada wa uzalishaji” wakisema kwamba "kuuza bidhaa nyingi katika soko la nje kunamaanisha uwezo wa ziada wa uzalishaji", "Uwezo wa uzalishaji wa China unazidi kwa kiasi kikubwa mahitaji ya soko la ndani la China na unazidi mahitaji ya soko la kimataifa."

Kauli hiyo haina msingi wowote.

Nicholas Lardy, mtafiti mwandamizi katika Taasisi ya utafiti wa uchumi wa kimataifa ya Peterson, ambayo ni taasisi ya washauri bingwa wa Marekani, amesema kuwa: "kauli hiyo inaonekana kumaanisha kwamba hakuna nchi inapaswa kuzalisha bidhaa zaidi ya uwezo wake wa mauzo ya ndani."

Kwa mujibu wa mantiki ya baadhi ya watu nchini Marekani na nchi nyingine za Magharibi, ikiwa uwezo wa uzalishaji wa nchi unazidi mahitaji yake ya ndani, ni “Uwezo wa ziada wa uzalishaji”. Basi, Marekani inauza nje kiasi kikubwa cha chipu, ndege, soya na bidhaa nyingine kila mwaka, na Marekani pia ina “Uwezo wa ziada wa uzalishaji”.

Je, kweli China inauza nje bidhaa nyingi zinazotumia nishati mpya?

Katika miaka miwili iliyopita, bidhaa hizo "tatu mpya" za China zimekuwa zikikaribishwa duniani kote, na kufikia ukuaji wa haraka wa mauzo ya nje. Hata hivyo, mauzo ya nje ya magari yanayotumia nishati mpya ya China ni sehemu ndogo ya jumla ya uzalishaji kuliko nchi kama vile Ujerumani, Japan na Korea Kusini. Kwa mfano, Ujerumani ilizalisha magari milioni 4.1 mwaka jana, ambapo milioni 3.1 kati yao yaliuzwa nje ya nchi, ikichukua karibu asilimia 80 ya jumla ya uzalishaji wake wa magari. Mwaka jana, China ilizalisha magari milioni 9.587 yanayotumia nishati mpya na kuuza nje magari milioni 1.203, ikiwa ni asilimia 12.5 tu.

Je, uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kijani wa China unazidi?

Chini ya hali ya uchumi wa soko huria, uwiano kati ya uzalishaji na mahitaji vinahusiana, na kutokuwepo kwa uwiano ni kawaida. Uzalishaji unaozidi mahitaji kwa kiwango kinachofaa unasaidia kukuza ushindani wa soko, kubaki sokoni kwa wale walio bora zaidi, kuhimiza uvumbuzi wa teknolojia na kupunguza gharama, pia inawasaidia wanunuzi wa nchi mbalimbali kupata bidhaa na huduma bora kwa gharama ya chini zaidi.

Bei ni kigezo muhimu katika kupima uzalishaji na mahitaji. Ikiwa China ina “Uwezo wa ziada wa uzalishaji” kama baadhi ya watu wa Marekani wanavyosema, bei ya bidhaa zinazotumia nishati mpya za China katika soko la kimataifa ingekuwa chini kwa muda mrefu. Hali halisi ni kwamba, kadiri mauzo ya nje ya magari yanayotumia umeme ya China yanavyoongezeka, ndivyo bei yake inavyoongezeka. Bei ya wastani ya magari yanayotumia umeme barani Ulaya ni takriban mara mbili ikilinganishwa na bei nchini China. Ongezeko la mauzo na bei linamaanisha kuwa uzalishaji wa magari haukidhi mahitaji ya sokoni. Tunawezaje kuzungumza juu ya "ziada ya bidhaa"?

Lazima tuwe na mtazamo wa kimataifa kuhusu masuala ya uwezo wa uzalishaji.

Hivi sasa, bado kuna nafasi kubwa ya ukuaji wa mauzo ya magari yanayotumia nishati mpya katika miji ya China ya ngazi ya tatu na ya nne na masoko ya vijijini. Baadhi ya wachambuzi wanakadiria kwamba kiwango cha magari yanayotumia nishati mpya nchini China kitaongezeka kutoka asilimia 35.2 Mwaka 2023 hadi asilimia 60 Mwaka 2033. Kwa maneno mengine, kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya maisha bora kwa watu zaidi ya bilioni 1.4 wa China hakutaachwa na maendeleo ya sekta nishati mpya, uboreshaji wa uwezo wa uzalishaji na viwango vya teknolojia. Hakuna anayestahili kukosoa hili.

Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Kimataifa la Nishati, mahitaji ya kimataifa ya magari yanayotumia nishati mpya yatafikia magari milioni 45 mwaka 2030, zaidi ya mara nne ya 2022; mahitaji ya kimataifa ya uwezo wa vifaa vipya vya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua yatafikia gigawati 820, takriban mara nne ya mwaka 2022. Mbali na kufikia kuwa "ziada" ya bidhaa za nishati mpya katika soko la kimataifa, kuna uhaba! Ikiwa nchi inayozalisha bidhaa nyingi za kijani, China inabidi kujiunga na kushiriki kikamilifu.

Ukweli ni kwamba, katika sekta ya nishati mpya, kampuni za China zinaendelea kutoa mchango kwa Dunia: huko Hungary, Kampuni ya magari ya BYD inajenga kiwanda cha uzalishaji wa magari yanayotumia nishati mpya hatua kwa hatua, ambacho kinakadiria kutoa maelfu ya nafasi za ajira kwa wenyeji; nchini Thailand, Changan, SAIC, BYD na kampuni nyingine za magari za China zinajenga viwanda, na uwekezaji wa jumla uliopangwa umezidi yuan bilioni 10.

Iwe kusafirisha bidhaa, kukidhi mahitaji ya soko la kimataifa, au kujenga viwanda nje ya nchi, kuchochea uwekezaji, kuhimiza ajira, na kupanua viwanda, kampuni za nishati mpya za China siku zote zinafuata kunufaishana, na maendeleo kwa pamoja. Hii pia imesifiwa na watu wengi wa kimataifa. Tovuti ya jarida la "Diplomat" la Marekani imebainisha kuwa nchi za Asia Kusini-Mashariki zinajitahidi kushirikiana na kampuni za magari yanayotumia umeme za China, "si tu kunaimarisha mageuzi ya lazima kutoka kwenye magari yanayotumia mafuta hadi magari yanayotumia umeme, pia inahimiza ukuaji wa uchumi kupitia mawasiliano ya teknolojia."

Kukosoa China kuwa na “Uwezo wa ziada wa uzalishaji” kunaficha nia mbaya ya kujilinda kibiashara. Mtazamo wa mfanyabiashara Mfaransa Bertrand amesema: "Suala la msingi katika kauli husika ni uwezo wa ushindani, si uwezo wa uzalishaji. Baadhi ya nchi za Magharibi zina wasiwasi kwamba China inaendeleza kwa kasi kubwa na kampuni za China zina uwezo mkubwa wa ushindani, jambo ambalo litatishia nafasi zao za uonogozi katika sekta husika. "

Kufungamanisha pamoja maendeleo ya sekta ya nishati mpya ya kimataifa na kujilinda kibiashara bila shaka kutadhoofisha uwezo wa nchi mbalimbali kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kukuza maendeleo ya kijani, na hatimaye itakuwa ni "kujipiga risasi wenyewe mguuni."

Biashara ya kimataifa siyo "mchezo wa kutonufaishana". Hakuna nguvu inayoweza kuzuia wimbi la utandawazi wa kiuchumi unaojumuisha watu wote na kuwanufaisha wote. Kwa ushirikiano wa wazi na kunufaishana, soko la bidhaa za kijani litakua kubwa zaidi na zaidi, na mustakabali wa jumuiya ya binadamu utakuwa bora zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha