Msaada uliotolewa na China wawasili Papua New Guinea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2024

Msaada uliotolewa na China kwa Papua New Guinea ukiwasili Port Moresby, Papua New Guinea, Aprili 25, 2024. (Ubalozi wa China nchini Papua New Guinea/ Xinhua)

Msaada uliotolewa na China kwa Papua New Guinea ukiwasili Port Moresby, Papua New Guinea, Aprili 25, 2024. (Ubalozi wa China nchini Papua New Guinea/ Xinhua)

SYDNEY - Vifaa vya msaada vilivyotolewa na China kwa Papua New Guinea vimewasili Port Moresby siku ya Alhamisi huku Balozi wa China katika nchi hiyo ya kisiwa cha Bahari ya Pasifiki, Zeng Fanhua akisema kuwa hatua hiyo itasaidia watu walioathirika kukabiliana na majanga ya asili ya hivi majuzi na kujenga upya nyumba zao.

Balozi Zeng na Waziri wa Ulinzi wa Papua New Guinea Billy Joseph kwa pamoja walishiriki kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jacksons wa Port Moresby.

Balozi Zeng amesema kuwa ikiwa ni mwenzi mzuri wa Papua New Guinea ambao watakuwa wakijaliana, China inaelewa hisia ya watu wa PNG wanaoathirika na majanga ya hivi karibuni, yakiwemo mafuriko na matetemeko ya ardhi.

Kwa niaba ya serikali na watu wa Papua New Guinea, Joseph ameishukuru China kwa msaada huo unaotolewa kwa wakati, akisema kuwa Papua New Guinea itasambaza vifaa hivyo kwenye maeneo yaliyokumbwa na maafa haraka iwezekanavyo.

“China siku zote imedumisha urafiki kati ya nchi hizo mbili na ni rafiki wa kweli wa Papua New Guinea”, Joseph amesema, huku kuongeza kuwa Papua New Guinea inaithamini sana na ingependa kuimarisha zaidi ushirikiano na China ili kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha