Naibu Waziri Mkuu wa China asisitiza uvumbuzi katika maendeleo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2024

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihutubia kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Zhongguancun Mwaka 2024 mjini Beijing, China, Aprili 25, 2024. (Xinhua/ Zhang Ling)

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihutubia kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Zhongguancun Mwaka 2024 mjini Beijing, China, Aprili 25, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

BEIJING - Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, pia mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Alhamisi wakati akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Zhongguancun la 2024 alisisitiza kwamba uvumbuzi ndio nguvu kuu katika maendeleo ya nchi.

Ding amesema China imetekeleza mkakati wa kupata maendeleo kwa kutegemea uvumbuzi, hivyo imepata mafanikio mapya katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na kuendeleza viwanda vya aina mpya, miundo mipya ya biashara na vichocheo vipya vya ukuaji wa uchumi, hayo yote yamekuwa kielelezo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Ameongeza kuwa Zhongguancun inatoa mchango mkubwa katika kuhimiza kazi ya kujitegemea kisayansi na kiteknolojia kwenye kiwango cha juu na kuujenga mji wa Beijing kuwa kituo cha kimataifa cha uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, na inapaswa kuendeleza zaidi mageuzi ya majaribio na kuharakisha ujenzi wa eneo maalum la sayansi na teknolojia la kiwango cha cha juu duniani.

China ingependa kujiunga na jumuiya ya kimataifa katika kutekeleza kwa vitendo kanuni za ushirikiano wa kimataifa katika sayansi na tekenolojia ulio " wazi, wenye haki na usawa na usiobagua", ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya dunia nzima ya sayansi na teknolojia, Ding amesema.

Ametoa wito wa kuhimiza jumuiya ya kimataifa kuunda kwa pamoja mfumo wa wazi wa uvumbuzi, kuandaa na kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, na kutatua matatizo makubwa ya kisayansi na teknolojia.

Mkutano wa mwaka wa jukwaa hilo la mwaka huu una kaulimbiu ya “Uvumbuzi Waijenga Dunia Bora Zaidi” Wadau karibu 1,000 wa kisayansi na kiteknolojia kutoka ndani na nje ya China, viongozi wa biashara, maofisa wa serikali, na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa walishiriki kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitembelea maonyesho baada ya kuhutubia ufunguzi wa Jukwaa la Zhongguancun Mwaka 2024 mjini Beijing, China, Aprili 25, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Naibu Waziri Mkuu wa China Ding Xuexiang, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitembelea maonyesho baada ya kuhutubia ufunguzi wa Jukwaa la Zhongguancun Mwaka 2024 mjini Beijing, China, Aprili 25, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha