"Uuzaji nje wa bidhaa za kijani za China hudhuru uchumi wa nchi zingine"? Hakuna mantiki!

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2024

Hivi karibuni, baadhi ya watu nchini Marekani wamekuwa wakivumisha juu ya kinachoitwa "uzalishaji wa kupita mahitaji ya soko" wa China katika nishati mpya, wakidai kuwa "China ina uzalishaji kupita mahitaji ya soko katika 'bidhaa tatu mpya za kijani' zinazowakilishwa na magari yanayotumia nishati mpya, betri za lithiamu na bidhaa za kuzalisha umeme kwa jua. Ili kuuza bidhaa zilizozalisha kupita mahitaji ya soko lake, China imekuwa ikiuza nje kiasi kikubwa cha bidhaa zinazopotosha uhalisia wa soko kudhuru uchumi wa nchi nyingine.

Je, ukweli wa mambo ni upi? Tunaweza kwenda kwenye Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China na kutazama shughuli hii ambayo ni ya kuwezesha ufahamu wa mwenendo wa biashara ya kimataifa.

Kuanzia Aprili 15 hadi 19, awamu ya kwanza ya Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China, yanayofahamika pia kwa jina la Maonyesho ya Canton, yakiwa na kaulimbiu ya "Bidhaa zinazoundwa kwa Teknolojia ya Hali ya Juu" yalifanyika kwa mafanikio, huku eneo la maonyesho ya magari yanayotumia nishati mpya na vyombo vya usafiri vinavyotumia teknolojia za kisasa likivutia umati mkubwa wa watu.

"Magari yanayotumia nishati mpya yameunda mtindo wa kimataifa, na China ni kiongozi wa kimataifa katika nyanja ya magari yanayotumia nishati mpya, kwa hivyo tunatumai kununua bidhaa zaidi za magari yanayotumia nishati mpya hapa." amesema Eliton, mnunuzi kutoka Ulaya.

Hadi kufikia Aprili 19, wanunuzi 125,440 kutoka nchi na maeneo 212 duniani kote walikuwa wameshiriki kwenye maonyesho hayo ana kwa ana ukumbini, ikiwa ni ongezeko la 23.2% kutoka katika kipindi kama hicho mwaka jana. Miongoni mwao, 22,694 ni wanunuzi wa Ulaya na Marekani, wakichukua 18.1% ya wanunuzi wote.

Kwa upande mmoja, baadhi ya watu kutoka nchi husika wanadai kuwa "Uzalishaji wa bidhaa za kijani wa China kupita mahitaji ya soko unadhuru uchumi wa nchi nyingine", na kwa upande mwingine, kuna ukweli kwamba "Dunia yote inavutiwa na teknolojia ya kijani ya China." Tofauti kati ya pande hizi mbili ni dhahiri, na ukweli unajidhihirisha.

Uzalishaji kupita mahitaji ya soko unamaanisha kuwa ugavi wa soko unazidi mahitaji. Lakini kwa kweli, kutokana na mwelekeo wa maendeleo ya kimataifa, nchi zote zinatafuta na kufuata kwa hamasa njia za maendeleo ya kijani na yenye kutoa kaboni chache. Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Kimataifa la Nishati, mahitaji ya dunia ya magari yanayotumia nishati mpya yatafikia magari milioni 45 Mwaka 2030, zaidi ya mara nne ya 2022; Mahitaji ya kimataifa ya uwezo wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua wa vifaa vipya yatafikia gigawati 820, takriban mara nne ya yale ya mwaka 2022. Kwa maneno mengine, uwezo wa sasa wa uzalishaji wa bidhaa za kijani haujafikia hatua ya ziada, bali kuna upungufu mkubwa. Neno "ziada" linatoka wapi?

Hebu tuangalie kwa mtazamo wa sheria za kiuchumi. Kwa mujibu wa nadharia ya ulinganifu wa uwezo wa faida, kama nchi inaweza kuzalisha bidhaa fulani kwa gharama ya chini, nchi nyingine hazipaswi kuweka vikwazo vya ushuru. Badala yake, zinapaswa kuagiza bidhaa hii na kuuza nje bidhaa kwa ulinganifu wa uwezo wa faida.

Mchango wa kijani wa China kwa uchumi wa dunia unaonekana kihalisia. Kutokana na hali ya ukuaji duni wa uchumi wa dunia na mfumuko mkubwa wa bei, China imetumia vizuri mnyororo kamili wa viwanda na kuipatia dunia bidhaa za kijani zinazowakilishwa na "bidhaa tatu mpya" zenye ubora mzuri, ufanisi wa hali ya juu na bei nzuri, ambayo si tu imepunguza shinikizo la mfumuko wa bei duniani, lakini pia inatoa uungaji mkono mkubwa katika uthabiti wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi, na inasaidia nchi duniani kote kutekeleza Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu ya 2030 na malengo ya Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kijani wa China ni uwezo wa hali ya juu na ni adimu kwa maendeleo ya kijani duniani.

Hebu tuangalie takwimu: Mwaka 2023, uwezo kuzalisha nishati mbadala wa vifaa vilivyofungwa upya duniani ulikuwa kilowati milioni 510, huku China ikichangia zaidi ya nusu; Bidhaa zenye ubora wa juu za nishati safi za China zinauzwa katika nchi na maeneo zaidi ya 200 duniani kote; China pia imeshirikiana na nchi na maeneo zaidi ya 100 katika miradi ya nishati ya kijani, ikitatua ipasavyo matatizo ya matumizi magumu na ghali ya umeme katika nchi na maeneo husika. Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati Mbadala inasema kuwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Wastani wa Gharama ya Umeme (LCOE) ya miradi ya kuzalisha umeme kwa upepo na kwa nishati ya jua duniani imepungua kwa zaidi ya 60% na 80% mtawalia. Sehemu kubwa ya mafanikio haya yanahusishwa na uvumbuzi, bidhaa na uhandisi wa China.

Watu wa kimataifa wenye ufahamu wa mambo wamesema kwamba "nadharia ya uzalishaji kupita mahitaji ya soko" inatoa kisingizio cha kujihami kiuchumi, na madhumuni yake ni kuzuia maendeleo ya sayansi na teknolojia na uboreshaji wa viwanda wa nchi zinazoendelea zikiwakilishwa na China, na kudumisha umwamba wa kiuchumi duniani wa nchi husika kupitia njia zisizo za haki. Hii itakosa uungwaji mkono na wengi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha