Madaktari wa China waweka kambi ya matibabu nchini Kenya

(CRI Online) April 28, 2024

Kenya Alhamisi iliwakaribisha madaktari bingwa wa matibabu ya jadi ya China (TCM) kutoka Mkoa wa Sichuan kusini magharibi mwa China, ambao walitoa huduma mbalimbali za matibabu kwa raia wa China wanaoishi katika nchi hiyo.

Madaktari hao sita wa China wamebobea katika fani mbalimbali, zikiwemo magonjwa ya ngozi, mifupa, tezi na homoni, shingo, na magonjwa yanayohusiana na umri.

Ikiandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Sichuan na Chongqing nchini Kenya na Chama cha Wafanyabiashara wa China katika Afrika Mashariki, hafla hiyo ilitoa huduma za matibabu ya acupuncture na vikombe wakati wa kliniki ya bure huko Nairobi, nchini Kenya.

Raia wa China wanaoishi nchini Kenya na wakazi wa eneo hilo walihudhuria kambi hiyo ya matibabu, wakionesha kutambua zaidi matibabu ya jadi ya China katika huduma za afya za kawaida.

Kama sehemu ya safari yao ya nje ya nchi, madaktari wa matibabu ya jadi ya China walitoa huduma za uchunguzi na matibabu na kuelezea faida zake kwa wakazi wa eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha